Kompyuta

Jinsi ya Kuzuia “Automatic Updates” Kwenye Windows 10

on

Windows hunakinisha na kusukuma sasisho moja kwa moja kwenye kompyuta yako ili kuhakikisha una programu za hivi karibuni na vipengele bora vya usalama.

Hakika kipengele hiki  kinawaokoa watumiaji wa Windows kwenye shida ya kuangalia na kufanya sasisho wenyewe, bado hakikubaliki katika baadhi ya matukio.

Hasa pale unapokuwa na kifurushi kidogo cha data au wakati baadhi ya sasisho zina sababisha mgogoro kati ya peripherals.

Mafunzo haya yatakuonyesha njia mbili za kuzuia au kuzima sasisho za Windows moja kwa moja; kupitia Wi-Fi na / au kupitia Ethernet.

Wi-Fi

Kuna njia rahisi ambazo unaweza kuzitumia kuzima sasisho ya moja kwa moja (automatic updates) ikiwa PC yako imeunganishwa na mtandao wa intaneti kupitia Wi-Fi. Ili kufanikisha hili andika Change Wi-Fi settings kwenye Start Menu au Cortana search box na bonyeza Enter.

Windows 10

Set Wi-Fi connection to Metered

Bonyeza Advanced Options na kisha weka “on” kwenye Set as metered connection.

Ethernet

Utaratibu wa kuzuia sasisho za moja kwa moja kwa wale wanaoingia kwenye mtandao kupitia Ethernet kidogo unahitaji utaalamu lakini sio kwamba haiwezekani.

Fungua Group Policy Editor tool kwa kuandika gpedit.msc katika Start Menu au Cortana search box na bonyeza Enter.

Group Policy Editor tool

Bofya kwenye Computer Configuration, shuka chini na kisha ubonyeze Administrative Templates. Kwenye orodha ya upande wa kulia, bofya mara mbili (double click) chaguo la All Settings.

Configure Automatic Updates option

Shusha chini chaguo za mipangilio (settings options) na bonyeza mara mbili kwenye Configure Automatic Updates. Bonyeza kwenye Disable radio na kisha bofya Apply kuwezesha mpangilio.

Disabled Automatic Updates

SOMA NA HII:  Listi ya Kampuni 10 za Kubeti Mpira Nchini Tanzania

Kiujumla si vyema kuzuia Windows Automatic Updates kwa kuwa unaweza kupishana na maboresho muhimu na sasisho za usalama. Fanya hivyo kama kuna ulazima wa kufanya hivyo.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.