Apps za SimuIntanetiMaujanja

Jinsi ya kutumia WhatsApp kama sehemu binafsi ya kuhifadhi Taarifa zako

Whatsapp ni programu ya kutuma ujumbe inayokuweka karibu kwa kuwasiliana na marafiki na familia. Inafanya kazi kwa haraka, inafanya kazi karibu katika kila simu (ikiwa ni pamoja na kompyuta ya mezani ) na Facebook haina mipango ya kudai malipo kwa watumiaji wa Whatsapp.

Umekuwa ukitumia WhatsApp maalumu kwajili ya kutuma ujumbe na kupiga simu ila kuna matumizi mengine ya kuvutia kwenye WhatsApp ambayo yanaweza kuongeza thamani ya app hii kwenye simu yako.Mbali ya kuwasiliana na ulimwengu wa nje, unaweza pia kutumia Whatsapp kwa:

  1. Kuchukua na kuhifadhi mawazo, maelezo, memo za sauti, “scanned documents” na kitu chochote kile katika sehemu binafsi ya kuhifadhi taarifa ambayo unaweza kuitumia ukiwa sehemu yoyote ile.
  2. Kuhamisha kwa haraka viungo vya mtandao (web links), nyaraka, viwambo(screenshots) na faili nyingine kati ya kompyuta yako na simu bila ya kujisajili kwa ajili ya huduma nyingine.

Wazo ni rahisi. Unatengeneza “virtual contact” mpya ndani ya Whatsapp na, kila kitu unachotaka kukihifadhi kwa faragha, unaweza tu kushare na hii “virtual contact”.

Haiwezekani kutuma ujumbe wa Whatsapp kwenye namba yako mwenyewe lakini kuna maujanja rahisi kutatua tatizo hili. Tengeneza kundi jipya la Whatsapp likiwa na mshiriki moja tu – wewe. Jinsi ya kutengeneza:

  1. Fungua WhatsApp kwenye simu yako na kuunda kundi jipya.
  2.  Ongeza mtu yoyote kutoka kwenye kitabu chako cha namba za simu kwenye kundi hili. Lipe kundi lako jina kisha hifadhi(save).
  3.  Sasa nenda kwenye kundi lako la WhatsApp, bonyeza kuangalia orodha ya washiriki.
  4. Bonyeza na kushikilia jina la mshiriki mwingine kwenye orodha hiyo na kisha muondoe kwenye kundi.
SOMA NA HII:  Kampuni ya mawasiliano ya Zantel kuigeuza Tanzania kuwa kitovu cha Tehama

Hivyo tu. Kitu ulichonacho sasa ni sehemu binafsi ya kuhifadhi vitu kwenye WhatsApp ambayo inaonekana kwako tu na inaweza kupatikana kwenye mtandao (desktop) na simu yako ya mkononi.

Kama unataka kuhamisha taarifa kutoka kwenye kompyuta kwenda kwenye simu , fungua web.whatsapp.com kwenye kompyuta, na kisha tuma mafaili kwenye kundi hili na mala moja yatapatikana kwenye simu yako.

Usisahau kutoa maoni yako kuhusu mbinu hii

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako