Jinsi ya kutumia simu au internet ya simu kama modem kwenye kompyuta


Una Kompyuta, Una Smartphone yenye Android OS na huwa unapata tabu kutumia simu yako wakati ukiwa busy na Kompyuta? leo hii nitawaonyesha namna nyingine rahisi kabisa ya kugeuza simu yako kuwa modem ili undelee
kurahisisha maisha yako na kufurahia kuwa na hiyo smartphone yako au tablet.

Jinsi ya kutumia simu au internet ya simu kama modem kwenye kompyuta

1. Kwa kutumia ‘USB’
Kabla ya yote kwanza hakikisha simu yako imeunganishwa na kompyuta yako kwa kutumia ‘USB cable’ (yaani uwe kama unachaji simu kwa pc). Sasa fungua simu yako kisha nenda hadi ‘settings’ katika sehemu ya wireless and network bofya ‘more settings’ halafu bofya ‘tethering hotspotand portable hotspot‘ kisha bofya ‘USB tethering’ alafu subiri kama sekunde thelathini sasa hapo upo tayari kutumia internet ya simu kwa kompyuta yako.

2. Kwa kutumia ‘WireLess’ (WiFi Hotspot)
Hatua zake ni kama za hapo juu ila zinatofautiana mwishoni. Kabla ya yote kwanza hakikisha kompyuta yako ina wireless ili kuweza kupokea. Sasa fungua simu yako kisha nenda hadi ‘settings’ katika sehemu ya wireless and network bofya ‘more settings’ halafu bofya ‘tethering hotspotand portable hotspot’ kisha nenda ‘portable wi-fi hotspot’. Subiri kwa sekunde kadhaa itakuwa tayari imedetect kwenye kompyuta yako.

Ila sasa hiyo wreless inakuwa inalindwa na namba za siri ‘default password’ kwa iyo ili kuziona bofya juu ya ‘portable wi-fi hotspot’ utakuwa na uwezo wa kubadili jina la wireless pamoja na password. Baada ya hapo nenda kwenye kompyuta yako utaona imedetect hapo connect kisha kazi ni kwako kuanza kuitumia.

Kwa Habari Zaidi Na Maujanja Mbalimbali Ya Teknolojia Endelea Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa Mediahuru Kila Siku Kwani Daima Tunaaminika Katika Teknolojia!

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA