Sambaza:

Baada ya simu mpya ya Samsung Galaxy S8 kutoka wengi wameonekana kupendezwa na muundo pamoja na uwezo wa simu hiyo kwa ujumla.

 

Lakini kilichopendeza zaidi kwenye simu hii ni uwezo wa kutumia simu hii kwenye kompyuta kwa kutumia kifaa kipya cha Samsung Dex.

Samsung DeX ni jibu la kipekee la kubadilisha smartphone yako kwa kukupata huduma sawa na kompyuta yako ya mezani kutoka na kuiongeza Galaxy S8 nguvu za kuchakata na kuleta tija ya hali ya juu,. Watumiaji wa Samsung DeX wanaweza kuona na kusahihisha taarifa kwa kutumia simu zao, na kurahisha ufanyaji kazi wa smartphone kuwa mzuri na wenye kasi.

Ukiwa na Samsung Dex unaweza kuchomeka simu yako ya Galaxy S8 au Galaxy S8+ na simu hiyo itakuwezesha kutumia simu yako kwa kutumia keyboard na mouse kifupi ni kwamba utapata uwezo wa kutumia simu yako kama kompyuta huku ukiwa na uwezo wa kutumia programu za Microsoft Excel, Microsoft PowerPoint, Adobe Photoshop Lightroom pamoja na zingine nyingi.

Haijaishia hapo unapotumia kifaa hicho bado unakuwa na uwezo wa kutumia simu yako kama kawaida huku ukipata uwezo wa kujibu na kuandika meseji kwenye programu yoyote, zaidi ni kwamba kifaa hichi cha Samsung Dex kimewezeshwa na programu ambazo zinauwezo wa kusaidia kutumia kompyuta yako yenye mfumo wako wa Windows moja kwa moja kwenye kifaa chako. Kifaa hicho pia kimetengenezwa na feni ambayo inauwezo wa kupooza kifaa hicho pale kinapo tumiaka kwa sana.

SOMA NA HII:  Jinsi ya kubadili mpangilio wa keyboard ya kompyuta kuwa Dvorak keyboard

Ili kutumia kifaa hicho unaweza kuchomeka kifaa hicho kwa kutumia waya za HDMI ambazo zinakupa uwezo wa 4K pamoja na sehemu ya Ethernet ambayo unaweza kutumia kuchomeka internet kwenye simu yako pamoja na mambo mengine pia kifaa hicho kinakuja na USB C port ambayo ni sehemu ya kuchaji kifaa chako. Kwa sasa kifaa hicho bado hakija tangazwa bei yake wala siku ya kutoka lakini pia kifaa hicho hakita uzwa pamoja na simu hiyo ya Samsung Galaxy S8. Endele kutembea Tanzania Tech tutakujulisha pindi kifaa hicho kitakapo toka.


Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako