Apps za SimuIntaneti

Jinsi ya Kutuma Mafaili ya Aina Yeyote kupitia WhatsApp

Je unatamani kutuma mafaili ya aina yeyote ile kupitia WhatsApp ? Ndio sasa inawezekana, toleo jipya la WhatsApp linamuwezesha mtumiaji kutuma faili la aina yeyote kwenda kwa mtu mwingine.

Toleo hilo jipya linapatikana kwa watumiaji wa simu za Android na iOS kupitia masoko ya apps. Mwaka jana waliwezesha utumaji wa mafaili ya mfumo wa .doc, PDF, .csv , .txt na .xls ila kuanzia sasa utaweza kutuma mafaili ya aina yeyote.

 

Hatua za kutuma mafaili ya aina yeyote kupitia WhatsApp

  1.  Katika eneo la kuchati bofya alama ya kutuma faili, kisha bofya Document.
  2. Badala ya kuona mafaili yale ya txt, pdf na mangine kama hayo kama zamani kuanzia sasa kama unatumia toleo jipya basi utaweza kuona na mafaili ya mifumo mingine pia. Bofya na kutuma.

 

Bado kiwango cha ukubwa wa mafaili unayoweza kutuma kipo chini, kwa kutumia WhatsApp Web (kwenye kompyuta) utaweza kutuma hadi faili la ukubwa wa MB 64 na kwa Android ukubwa mwisho ni MB 100 wakati kwa watumiaji wa iOS (iPhone) wataweza kutuma hadi faili la ukubwa wa MB 128.

Je umeyapokeaje mabadiliko haya ya Whatsapp ? Kumbuka kushare makala hii na rafiki zako.

SOMA NA HII:  Vidokezo 8 rahisi jinsi ya kukuza tukio lako kwenye LinkedIn
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako