Jinsi ya kurudisha Mafaili Yaliyofutwa Katika Kompyuta


Je! Umewahi kuwa katika hali ambayo kwa bahati mbaya umefuta faili kwenye kompyuta yako? Hii inaweza kutokea wakati unafuta faili kwenye recycle bin kwenye Windows OS au wakati hatujazifanyia backup faili zetu na kuzipoteza kutokana na mashambulizi ya virusi au mambo mengine. Usiwe na hofu tena kwa sababu kuna suluhisho kwa ajiri kwako.

kompyuta

Faili zako hazifutiki moja kwa moja unapozifuta kwenye PC yako

Unajua kwamba kila unapofuta faili kwenye hard disk, faili hizo bado huendelea kuwepo na huwa hazifutiki kabisa? Windows OS pamoja na Mifumo Mingine ya Uendeshaji haifuti vitu vilivyomo ndani ya faili pale unapofuta faili hilo. Wanafanya hivyo ili kuokoa muda na kuongeza utendaji wa mfumo.

Mifumo ya Uendeshaji inachofanya ni kufuta pointer ya faili – aina ya data inayoonyesha eneo la faili – na faili lenyewe bado linaendelea kuwepo kwenye diski ngumu (hard disk) yako.

Jinsi ya kurudisha mafaili yaliyofutwa kwa kutumia EaseUS Data Recovery Wizard

Kuna programu nyingi za kurejesha data zinazopatikana kwenye mtandao ili kurejesha faili zako zilizofutwa, lakini katika mwongozo huu wa mafunzo, tutatumia EaseUs data recovery wizard.

Kurejesha data zako zilizofutika kwa kutumia EaseUs data recovery tool,fuata hatua hizi:

  • Hatua ya 1: Shusha (download) na pakua (install) programu hii kutoka kwenye mtandao (inapatikana kwa Windows na Mac OS). Toleo la majaribio (trial version) linaweza  kuscan faili zote zilizopotea. Kurejesha data zako, unatakiwa kuwa na license key.

  • Hatua ya 2: Ifungue programu kwenye PC yako.
  • Hatua ya 3: Chagua disk au partition ambayo unataka kurejesha mafaili yaliyofutika na kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa scan ipo chini kabisa.

Chagua drive ambayo umefuta faili

  • Hatua ya 4: Itaanza  kusoma kwa haraka (quick scan) kwa faili zilizofutwa, baada ya hapo ufuatiliaji wa kina (deep scan) utafuatia moja kwa moja kupata faili zaidi.

Deep scanning

  • Hatua ya 5: Hapa baada ya deep scanning utaona chaguo la ku-Preview au kurejesha faili zilizofutika.

Kurejesha Mafaili yako

  • Hatua ya 6: Hakikisha kwamba huhifadhi faili zilizopatikana kwenye drive au partition ile ile zilipokuwepo mwanzo kabla hazijafutwa .

Ni hayo tu.

Kumbuka kwamba unaweza kurejesha faili za kwenye hard-disk drives (HDDs) tu na si kwenye solid-state drives (SSDs) kwa sababu faili zinafutika moja kwa moja kwenye SSDs tofauti na HDDs.

Mwongozo huu unaweza kuwa na manufaa sana pale unapoteza faili zako na hauwezi kupata njia yoyote ya kuzirejesha. Natumaini umeipenda ? Usisahau kuandika maoni yako hapa chini.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA