Jinsi ya Kurudisha Data Zako Zilizofutwa Katika Simu ya Android


Kwa bahati mbaya unaweza kufuta taarifa zako muhimu kama vile picha au hata video na ukashindwa kuelewa ufanye nini kurudisha data zako, USIKASIRIKE sio kitu kipya wote tumeshawahi fanya. Mediahuru inakuletea njia ya kurudisha data zako kwenye kifaa cha android.

Ndiyo, unaweza kuzipata taarifa zako zote ambazo ulifuta kwa bahati mbaya lakini kabla ya kuzipata kuna mambo inabidi uyafanye:

  • Usihifadhi (save) kitu kingine chochote katika simu kifaa chako au izime mpaka ukiwa unampango wa kufufua vitu vyako.
  • Zima WiFi na njia za mawasiliano za 2G/3G ili masashisho (update) yanayofanyika automatic yasifanyike. Kumbuka kama yakifanyika, mafaili mapya yanaweza jiweka juu ya yale ambayo unataka kuyafufua

Zifahamu Njia Za Kurudisha Data Zako Zilizofutwa Katika Kifaa Cha Android

 Recuva Ikiwa Inafanya Kazi Yake

Kama Mafaili Yako Yapo Katika Memori Kadi
Ukishaona mafaili yako yamefutika bahati mbaya – au hata kwa makusudi – kitu unachotakiwa kufanya ni kuunganisha kompyuta yako na simu kwa kutumia USB. Kuna baadhi ya matoleo ya vifaa vya android, ukichomeka USB katika kompyuta haijionyesha katika mfumo ule wa ‘kuonekana kama umechomeka Flash tuu’ .

Kama simu yako haifanyi hivyo na una uhakika taarifa zako hizo zilikuwa katika sehemu ya memory kadi unaweza ukatumia adapta ya memori kadi hiyo na kuichomeka katika kompyuta ili isome mafaili yaliyomo ndani.

Sasa unatakiwa kushusha programu ya Recuva katika kompyuta (Unaweza ukashusha ya bure au ya kulipia). Bofya hapa Kushusha Recuva.

Ukishafungua Recuva kitu cha kwanza ni kuchagua mafaili gani unayotaka kuyafufua katika kifaa chako (picha, video n.k).

Unaweza ukachagua sehemu husika ambapo unataka mafaili ya eneo hilo yafufuliwe. Kitu cha muhimu cha kuweka akilini hapa ni kwamba program ya Recuva itaonyesha maeneo ambayo inaweza fufua mafaili yaliyofutika tuu.

Recuva ikionyesha mafaili ambayo unaweza ukayafufua (Itakubidi kuweka alama ya vyema katika mafaili unayotaka uuyafufua).

Kingine cha muhimu ni kwamba unashauriwa kama ukimaliza kufufua mafaili yako inabidi kwanza uyahifadhi (save) katika eneo lingine na kisha baadae ndio uyahamishie katika kifaa chako pale yalipofutika. Kujaribu kuyarudishia pale pale wakati unayafufua kunaweza kukaleta shida wakati mwingine. Kwa mfano kama ukiwa unafufua mafaili yako katika simu janja huna budi kuyahifadhi katika kompyuta yako na yakimaliza kufufuka uyapeleke tena katika simu.

Kama Mafaili Yako Hayapo Kwenye Memori Kadi (Yapo Kwenye Simu)
Kama mafaili unayotaka kuyafufua yalikuwa katika simu na sio memori kadi basi unaweza kutumia njia hii. Kama hujaruhusu njia chaguo la ‘Developer’ katika simu yako fanya hivyo kwa kwenda kwenye Settings > About Phone > Build Number au kwa simu zingine Settings > About Device > Build Number na kisha bofya katika eneo la namba hiyo (Build Number) mara 7.

Ukishamaliza kufanya hivyo nenda katika Settings > Developer Options And USB Debugging. Mpaka hapo utakuwa na uwezo wa kutumia programu kama Recuva katika kufufua mafaili yako.

Mpaka hapo nadhani utakuwa umepata msaada wa jinsi ya kurudisha vitu vyako. Vile vile niandikie hapo chini sehemu ya comment ni njia gani wewe unatumia kurudisha data zako zilizopotea kwenye vifaa vya Adroid?

Kwa Habari Zaidi Na Maujanja Mbalimbali Ya Teknolojia Endelea Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa Mediahuru Kila Siku Kwani Daima Tunaaminika Katika Teknolojia!

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA