Sambaza:

Baada ya kuinstall Windows au kubadilisha “monitor” yako unaweza kukutana na tatizo la kuonyesha (display problems).

Video zinaweza kuwa hazichezi kwenye high resolutions au programu (kama vile video games) inaweza kushindwa kuinstall, na kutoa ujumbe wa low graphics memory.

Mara nyingi, tatizo linaweza kuwa ni drivers. Drivers kimsingi ni programu na maelekezo ya jinsi vifaa (peripherals) vinavyoingiliana na mfumo wa uendeshaji.

Peripheral kama monitor, isipopata seti ya maagizo yake maalum, haiwezi kufanya kazi kama inavyotakiwa.

Kuna njia mbili unaweza kuboresha drivers za kompyuta yako; uiache kompyuta itafute yenyewe moja kwa moja au kupakua.

Ili kuweka moja kwa moja (install automatically):

 • Bofya mara mbili kwenye icon ya Control Panel kwenye skrini ya kompyuta yako. Kama huioni, andika ‘control panel’ kwenye Cortana na bofya kwenye chaguo la kwanza (app) inayoonekana kwenye orodha ya matokeo ya utafutaji.
 • Chagua chaguo la Hardware and sound na kisha chagua Device Manager.
 • Vinginevyo, bofya kwenye icon ya This PC kwenye desktop, chagua properties kisha fungua Device Manager.
Windows

Windows Device Manager

 1. Device manager itaonyesha orodha ya vifaa vilivyounganishwa kwenye PC yako. Sehemu yenye tatizo lazima iwe na alama ya njano ya kiulizo pembeni yake.
 2.  Right click na uchague Update Driver Software.
 3. Katika skrini inayofuata chagua Search automatically for updated software.

Driver search options

PC yako itatafuta drivers sahihi na kuziunganisha moja kwa moja. Ili mabadiliko yafanye kazi unatakiwa kurestart kompyuta yako.

SOMA NA HII:  Jinsi Data Zinavyohifadhiwa kwenye Diski Kuu na Umuhimu wa Kufanya Defragmentation

Ku-install wewe mwenyewe:

 1. Je! Kompyuta inashindwa kupata driver, kama ni hivyo unaweza kutumia njia hii ya kupakua kutoka kwa watengenezaji wa monitor yako.
 2. Hakikisha una onyesha jina halisi na model ya monitor yako ili kupata drivers zake sahihi.
 3. Mara baada ya kupakuliwa, fungua device manager kwa kutumia hatua nilizoweka hapo juu na uchague chaguo la kusasisha programu ya driver.
 4.  Badala ya kuruhusu kompyuta kufuatilia moja kwa moja, hapa chagua Browse my computer for driver software.
 5.  Fungua sehemu ulipoweka faili la driver ulilipakua na kisha bofya ok.
 6.  Baada ya driver kuwekwa kwa ufanisi anzisha upya mfumo (restart system).

Sasa utakuwa na uwezo wa kutumia monitor yako kwenye higher resolutions.


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako