Jinsi ya Kuongeza Nafasi Kwenye Kompyuta


Watumiaji wengi wa Kompyuta wamekuwa na hamu ya kuongeza nafasi kwenye kompyuta zao na vile vile kuweka nyaraka na taarifa zao nyingine katika mazingira bora ambapo anaweza kuzitumia muda wowote anaoutaka bila kulazimika kutumia muda mrefu .

kuongeza-nafasi-kompyuta

Hapa chini ni maelezo mafupi ya jinsi ya kutengeneza nafasi hizo na kuweka kompyuta yako katika mazingira bora ya matumizi .

katika uhifadhi wa vitu ni kwa njia ya mtandao kwa kutumia mawasiliano ya mfumo wingu , kwa njia hii unaweza kutumia taarifa zako ukiwa popote duniani kama umeunganishwa na mtandao pia unaweza kualika washirika kuangalia taarifa hizo , kuchukuwa au kufanya mabadiliko .

SOMA NA HII:  Mwalimu aliyechora ‘Microsoft Word’ kwenye ubao, apewa shavu

1. Gawa HDD ( Hard Disk ) sehemu mbili au zaidi .

Kompyuta inavyokuwa mpya mara nyingi inakuwa na partition moja ile inayoitwa C pekee , kwa matumizi bora ya kifaa chako unatakiwa ugawe upate “C” ambayo ndio yenye mfumo endeshi (operation system) , “D” ambayo inaweza kuwa kwa ajili ya Data na “E” ambayo unaweza kuweka iwe kwajili ya backup. Hii itafanya uweze kupanga vitu kwa mfumo mzuri.

Kusoma makala yetu yenye ufafanuzi wa jinsi ya kugawa partition bila ya kutumia programu bonyeza hapa.

2. Faili za Muda ( Temporary Files )

Kila unapofanya jambo fulani kwenye kompyuta yako basi faili za muda hujihifadhi sehemu , unaweza ukaziona au usione lakini kadri unavyoendelea na matumizi faili hizi huwa kubwa na nyingi zitajaza nafasi zinatakiwa kuondolewa kabisa.

SOMA NA HII:  Jinsi ya kubadili mpangilio wa keyboard ya kompyuta kuwa Dvorak keyboard

kuongeza nafasi

Unaweza kufuta faili za muda mfupi kwa kuandika RUN kwenye sehemu ya utafutaji ya kompyuta yako. Baada ya hapo ifungue na kuandika neno hili %temp%, kisha bonyeza OK utaona faili nyingi unaweza kuzifuta kwa sababu zinatumia nafasi kwenye kompyuta yako bila ya kuwa na umuhimu.

3. Faili Kujirudia ( File Dublicates )

Kama wewe ni mpenzi wa muziki saa nyingine unaweza kuhifadhi miziki inayojirudia rudia , au kama ni faili zinazojirudia rudia , hii hujaza nafasi kwenye hifadhi ya komputa yako , kuna programu maalumu za kuondoa faili zilizojirudia na kuwa na moja tu programu hizi nyingi ni bure unaweza kuzipata kwa njia ya mtandao .

SOMA NA HII:  Baada ya kashfa thamani ya facebook yashuka kwa $58bn

4. Matumizi ya Antivirus

Kuna aina za Virus zinazoathiri kompyuta kwa kujigawa mara mbili au zaidi ya hapo , hawa hawawezi kutoka kwa kutumia Disk Cleanup au Hatua ya 3 hawa wanatoka ukiwa na Antivirus iliyokuwa updated ili kuondoa athari hiyo.

MWISHO

Njia nilizozitaja hapo juu zinaweza kufanya kazi kwa uzuri zaidi kama kompyuta yako haina matatizo mengine yanayohusiana na Vifaa vilivyochomekwa au Programu zilizomo kwenye kompyuta hiyo au Kuathiriwa na Virus .

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA