Android

Jinsi ya kuongeza kasi ya simu yako ya Android

on

Leo, nitakuonyesha njia 6 zilizothibitishwa za kufanya simu yako ya Android iwe na kasi zaidi.

simu yako ya Android
Angalia njia 6 za kuongeza kasi ya simu yako ya Android  hapa chini: –

1. Futa Apps usizozitumia

Apps usizozitumia zinafanya nini kwenye simu yako, zifuta ili uongeze nafasi … nenda kwenye settings > applications

2. Restarting simu yako kila asubuhi

Kuanzisha upya simu yako ya android, hupunguza sehemu ya memori iliyokuwa inatumiwa na programu zilizokuwa zimezifunguliwa.

3. Futa Programu Zisizofaa

Watu wengi wanapenda kuweka (install) apps nzuri na mbaya kwenye simu zao za android na kuiita “swag”, simu yangu ina apps nyingi, bila kujua wanaua simu. Kwa mfano, umeweka antivirus ya AVG, AVAST Mobile Security, Netqin, haha, unahitaji nini kwa kutumia antivirus 3 ?? hun? Weka programu za kawaida unazozitumia mara kwa mara. Fanya simu yako iwe ya wastani.

SOMA NA HII:  Njia 5 zitakazokuwezesha kutumia simu wakati unaendesha gari

4.Sasisha (update) Anti-Virus yako

Sasisha antivirus yako na daima “scan” simu yako, inaweza kuwa kila siku kabla ya kwenda kulala, baadhi ya antivirus zina sifa hiyo, kufanya “auto scan” kwenye simu kwa kuweka muda maalumu wa kufanya hivyo.

5.Weka Apps kwenye Memory Card (SDCard)

Hifadhi apps kwenye kadi ya kumbukumbu ili kuongeza nafasi kwenye simu yako ya mkononi, ili simu iweze kufanya kazi muhimu kwa urahisi.

6.Futa Ujumbe uliousoma au Kuutuma

Nashangaa kwa nini watu wengine wanahifadhi sms kutoka kwa watoa huduma kama airtel, tigo, halotel na Vodacom. Unatakiwa kujua kuwa sms kutoka kwa mtoa huduma huchukua hadi “35kilobytes” na unapoendelea kuziweka na kufikia “28messages” ni kwamba umetumia karibu 1MegaByte, hivyo ni muhimu kufuta sms kwenye inbox yako.

SOMA NA HII:  Simujanja Unlocked: Maana ya Processor na Kazi Yake Kwenye Simu

Ikiwa una njia zingine za kuongeza kasi ya simu yako ya android , tunaomba utujulishe kwa kutoa maoni kuhusu makala hili.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Reply

Your email address will not be published.