Tunaishi wakati ambao watu mara nyingi huchagua simu zao juu ya marafiki zao. Muda ambao ikiwa tukio halijawekwa kwenye mitandao ya vyombo vya habari vya kijamii (social media networks), basi halikutokea.

Wengi wetu tunafurahia urahisi wa kuunganishwa kwenye mtandao, kwa kutumia simu za mkononi kupakua apps, live stream videos, kununua vitu mtandaoni au hata kuangalia habari imekuwa kawaida – tunapenda uwezo wa kuunganishwa mara moja na ‘ulimwengu ‘ Kutoka kwenye viganja vya mikono yetu. Hata hivyo, wengi hawajawahi kufikiria watafanya nini watakavyoshambuliwa na cyberattack wakati wameunganishwa na mtandao. Kwa kuzingatia kwamba watu karibu bilioni 3.7 hutumia Intaneti – wengi wanaweza kufikiri kuwa nafasi y wao kuathiriwa ni ndogo, na hivyo hawalindi taarifa zilizomo kwenye simu zao.

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kugawa Partition Kwenye Windows bila "Kuformat"

Wakati watu wanaamini kwamba hili haliwezi kutokea kwao – ukweli ni kwamba watumiaji 10,000 wa Facebook ulimwenguni, walishambuliwa na malware ndani ya siku mbili na kufanikiwa kuvamia akaunti za Facebook, mwaka jana. Kwa hiyo, ungefanya nini ikiwa umepoteza taarifa zako zote, anwani, picha na video kwenye simu yako? Ungewezaje kurudisha (recover) taarifa au uhakikishe kuwa taarifa zilizopotea zinalindwa?

Hivi vidokezo vitatu vitakusaidia kukukinga wewe na smartphone yako ili uweze kufurahia muda wako mtandaoni – bila wasiwasi:

1. Weka (install) app nzuri ya usalama wa mtandao

App nzuri ya usalama wa Intaneti kwajili Android, inakupa uhuru wa kutumia mtandao kwa usalama. Sio tu app ya usalama kuzuia internet scams au vitisho kutoka kwa cybercriminals ambao wanaweza kutaka kuiba taarifa zako binafsi kwa faida yao wenyewe, lakini pia itazuia scams/threats vingine vinavyozunguka mtandaoni – kwa mfano, hakuna mtu anaweza Kujifanya kuwa wewe kwenye mitandao ya kijamii au app zingine za kuchat.

SOMA NA HII:  Simujanja Unlocked: Maana ya Processor na Kazi Yake Kwenye Simu

2. Daima angalia url

Cybercriminals wanajaribu kuunda tovuti bandia za bidhaa maarufu. Wakati tovuti hizi zinaonekana halisi, daima angalia bar ya url ya kivinjari chako. Unapaswa kuona ‘https’ – si ‘http’ – mwanzoni mwa URL, na ishara ndogo ya kufuli karibu nayo. Hii ndio ishara inayokuambia kwamba tovuti hii ni salama kutumia na sio bandia iliyowekwa ili kuiba taarifa za kibinafsi unapoingia.

3. Usipakue tu app – fanya utafiti

Kama vitu vingine vyote, fanya zoezi hili. Hakikisha unaangalia taarifa zote kuhusu app yoyote unayotaka kupakua – kwanza. Angalia ni nani “publishers” wake na maoni ya watu kuhusu app hiyo, hii itakuambia ikiwa app nzuri kwajili ya smartphone yako. Pia, daima kupakua kutoka kwenye duka la app store/platform inayoaminika.

SOMA NA HII:  Majibu 9 ya maswali unayojiuliza kuhusu Teknolojia ya sasa

Daima ni bora kuchukua hatua za kuzuia kabla smartphone yako kuambukizwa, cybercriminals siku zote wanajaribu kutafuta njia mpya ya kukudanganya kuwa mwathirika wa cybercrime. Kuwa makini na endelee kujilinda!

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako