Sambaza:

Unroll.me ni huduma ya bure mtandaoni ambayo inakuwezesha kujitoa kwa urahisi katika barua pepe na ujumbe mwingine kwenye Gmail. Hata hivyo, unatakiwa kutoa ruhusu kamili kwenye mailbox yako ya Gmail na Anwani yako ya Google(Google Contacts) kwajili ya Unroll.me kuwa na uwezo wa kuondoa moja kwa moja anwani yako ya barua pepe kutoka kwenye orodha ya barua mbalimbali.

Kama unahofu kuwa, Unroll.me inaweza kuendelea kuingia kwenye email yako siku zijazo. Huu ni mwongozo rahisi wa jinsi ya kuzuia programu hii kutumia barua pepe yako ya Gmail katika siku zijazo.

Hii ni “automated system” nyingine kwajili ya kuitoa anuani yako ya Gmail address kutoka kwa “bulk senders”. Huu ni mwonekano wake:

Jinsi ya Kujiondoa kwenye Email Zinazotumwa kwenye kwenye Gmail

Kitu ninachokupa sasa ni “Google Script” rahisi ambayo  inaangalia yaliyomo kwenye “bulk emails”  na kutafuta kiungo (link) ya kujitoa. Kama link ya kujitoa inapatikana, script hii inafungua kiungo hicho na barua pepe yako moja kwa moja inakuwa imejiengua. Wakati mwingine, mtumaji wa bulk anahitaji utume ujumbe kwenye barua pepe maalumu ya kujitoa na script yetu ya Google inaweza kufanya hivyo pia.

Faida kubwa ni kwamba hautakiwi kutoa ruhusa ya kuingia kwenye akaunti yako ya Gmail kwa huduma yoyote ile (third-party service) na unaweza kuongeza barua pepe ya kujisajili kwenye foleni ya kujitoa kutoka kwa mteja yoyote wa barua pepe ikiwa ni pamoja na desktop na programu za simu. Tuanze:

  1. Bonyeza hapa kucopy “Gmail Unsubscriber sheet” kwenye hifadhi ya Google(Google Drive)
  2. Nenda kwenye Gmail menu ndani ya Google Sheet (angalia screenshot hapo juu) na chagua Configure. Ruhusu script kutumia akaunti yako ya Gmail. Ni open source Google Script inayofanya kazi bila ya kuhifadhi ama kupakia(upload) taarifa zako kabisa.
  3. Kwenye sanduku la inbox, andika jina la Gmail label yako (chaguo-msingi ni Unsubscribe) na barua pepe zote zenye alama ya “label” hii zitakuwa zimeondolewa. Hifadhi mabadiliko yako.
SOMA NA HII:  Vidokezo 8 rahisi jinsi ya kukuza tukio lako kwenye LinkedIn

Programu ya Gmail Unsubscriber sasa imewezeshwa na inafanya kazi nyuma ya pazia. Sasa unaweza kutumia Unsubscribe label kwenye ujumbe wowote ule wa barua pepe katika Gmail na moja kwa moja utakuwa umejiondoa ndani ya dakika 10-15. Kila kitu kipo kwenye “Google sheet”  kwa hiyo unakuwa unajua nini kinatokea nyuma ya pazia. Hebu jaribu programu hii!

Pia, ufumbuzi huu unafanya kazi kila mahali – unaweza kuitumia kwenye “subscription newsletters” usizozihitaji kwenye tovuti ya Gmail, programu za simu za Gmail kwenye iPhone na Android au kwenye kampuni zingine za email kama Microsoft Outlook (weka barua pepe kwenye Unsubscribe folder) au Apple mail.


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako