Jinsi ya kuhamishia Apps katika Memori kadi #Android


Je unataka kujua jinsi ya kuhamishia app kwenye memori kadi ili kuweka vitu vingine kwenye simu? Maana simu nyingi zinazotumia android OS zina sehemu ya kuweka Memori Kadi (memory card slot) kumwezesha mtumiaji kuongeza nafasi ya ziada ya kuhifadhi data.

kuhamishia app

Ikiwa simu yako ina Diski ujazo (Internal Storage) ndogo, kuweka games au apps kwenye simu hiyo inaweza kupunguza utendaji wake.

Ili kuepuka hali hii, unatakiwa kuhamishia Apps na Games katika Memori kadi ambayo umeiweka kwenye kifaa chako.

Pia inategemea aina ya Memori Kadi utakayoitumia. Ni vizuri kuweka iliyo na nafasi kubwa zaidi. Kuanzia 10 GB na kuendelea itakupa nafasi nzuri ya kuweka App nyingi uzipendazo.

Hizi ni hatua ambazo zitakuwezesha kuhamishia App zote katika Memori kadi bila kutumia programu yoyote.

1.Nenda kwenye Setting

2.Kisha Apps (Baadhi ya simu panasomeka application manager au Manage Apps)

3.Chagua App utakayopenda kuihamishia katika Memori Kadi

4.Bofya Storage.

5.Bonya sehemu iliyoandikwa “Change” kama ipo. Kama hakuna sehemu pameandikwa ‘Change’, ujue app hiyo haihamishiki. Ikiwa kila app unayojaribu kuhamisha haina chaguo hili, inawezekana kuwa simu yako haina uwezo wa kuhamisha apps.

6.Bofya Move.

Ikiwa unataka kurudisha tena app kwenye internal memory, Bofya tena sehemu iliyoandikwa “change” na chagua Uhifadhi wa ndani (Internal Storage).

Kumbuka, sio simu zote za Android zinakuwezesha kuhamishia app kwenye memori kadi , lakini kwa zile zenye uwezo huu ni mchakato wa haraka na rahisi kwa mtumiaji.

Kwa wale ambao wanatumia toleo la Android Nougat 7.0 na kuendelea wanaweza kuseti moja kwa moja kwenye Memori Kadi kila wakiinstall App inakwenda katika Memori Kadi.

Lakini kumbuka unapoweka App katika Memori Kadi usijaribu kuitoa ndani ya simu, kwani kufanya hivyo utashindwa kuzitumia App hizo mpaka utakapoiingiza tena katika simu.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA