Jinsi ya kugundua (na kuepuka) barua pepe za udanganyifu


Inaonekana kwamba wadanganyifu (fraudsters) siku hizi kwenye mtandao wapo kila mahali , na wengi wao hutuma spam kama ujumbe unaoingia kwenye barua pepe zetu kila siku. Na wapo vizuri sana kutengeneza ujumbe wa kuvutia zaidi, na wa kuaminika pia.

Ikiwa umetumia Intaneti, hakika umewaona wengi sana. Maandishi yao mara nyingi hudai kuwa ni kutoka kwa benki yako, PayPal, Amazon, Facebook au shirika lingine la mtandao ambalo lina uhalali wa kuweka habari zako za kifedha kwenye faili zao.

Lengo la wadanganyifu hawa kawaida ni kukufanya wewe ubofye link kwenye barua pepe ambayo inakupeleka kwenye tovuti bandia, lakini huonekana kama tovuti halisi. Kama barua pepe yenyewe, tovuti bandia itaonekana ya kweli kabisa, imekamilika pamoja na logo na mara nyingi taarifa za mawasiliano halali. Kwa kweli, tovuti bandia itaonekana karibu sawa na tovuti halisi ya kampuni. Lakini hapo ndio mwisho wa kufanana.

Unapojaribu kuingia (log in) kwenye tovuti bandia utagundua kwamba fomu ya kuingia (login form) haifanyi kazi. Utaona tu ujumbe halali wa hitilafu  baada ya kuandika jina lako na nenosiri lako – lakini kwa wakati huo crook tayari imenakili taarifa zako za kuingia (login credentials). Atachukua maelezo yako ya kuingia aliyoiba na kuingia katika akaunti yako kwenye tovuti halisi na kukuweka katika usalama mdogo.

Watu wasio na idadi wanaingia kwenye mtego huu wa barua pepe hizi za ulaghai (fraudulent emails) kila mwaka, lakini huna haja ya kuwa mmoja wao kwa sababu ni rahisi sana kugundua. Ni hivi:

  1. Barua pepe kamwe haitatumwa kwako moja kwa moja. Badala yake, mara nyingi husema kitu kama “Hello, valued PayPal customer”.  Wakati mwingine itaonyesha ni kwajili yako kwa anwani yako ya barua pepe. Kwa upande mwingine, barua pepe halali itakuja kwa jina lako.
  2.  Maudhui ya ujumbe wenyewe mara nyingi hutumia Kiingereza kisichoeleweka vizuri kama imeandikwa na mtu ambaye sio mwongeaji wa Kiingereza (na mara nyingi labda kwa sababu barua pepe nyingi za ulaghai zinatoka nje ya nchi).
  3.  Utaombwa kubofya link ili kutembelea tovuti ya kampuni ili kusasisha au kuthibitisha taarifa zako za mawasiliano na / au credit card au maelezo ya akaunti ya benki.

Ikiwa unahisi kuwa barua pepe ni ya udanganyifu lakini huna uhakika, usibofye link yoyote iliyo kwenye barua pepe. Badala yake, tembelea tovuti moja kwa moja (ikiwezekana kutoka kwenye bookmark  ambayo umetumia zamani) na uingie kwenye akaunti yako kutoka huko. Ikiwa kuna kitu ambacho hakika kinahitaji kufanyiwa update, utambiwa mara tu unapoingia,

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA