MaujanjaWindows

Jinsi ya kufuta folda ya Windows.old na kuongeza nafasi kwenye kompyuta

Kuhamia kwenye Windows 10 huleta vipengele vipya kwenye mfumo wa uendeshaji (operating system) wa Microsoft – baadhi ni muhimu zaidi kuliko vingine. Windows 10 ni mfumo wa uendeshaji imara ambao umeendelea kupokea marekebisho mazuri na kuongezwa vipengele bure bila malipo tangu kutolewa kwake ikiwa unahama kutoka kwenye Windows 7 au 8.

Baada ya sasisho unaweza kuona baadhi ya icons na njia za mkato (shortcuts) zimefutwa, kama kuongezwa tena kwa Windows Store au icon ya kivinjari cha Edge kwenye taskbar .

Sasa, jambo ambalo halipo wazi ni kwamba update kubwa inafanyika kama kuboreshwa kwa Windows (kubadilisha windows). Ili kuweka vitu sehemu salama, usanidi wa Microsoft unahifadhi nakala kamili ya Windows unayoitumia hivi sasa (hiyo ni folda ya Windows.old ), folda la Windows.old lina umuhimu pale linapotokea tatizo kwenye kuweka mfumo mpya na inakulazimu kurudi kwenye mfumo wa zamani, pia hutumia nafasi kubwa “gigabytes” kuhifadhi faili hizo.

Hii sio Windows 10 mpya, lakini ni faili kamili la kufanya “backup” . Ikiwa bado una nafasi kubwa kwenye kompyuta yako basi usiangaike kufuta folda hili maana litajifuta lenyewe moja kwa moja siku 30 baada ya sasisho. Ikiwa unataka kurudisha mfumo wa zamani, kufuta folda hii kunaondoa fursa hiyo mikono mwako.

Lakini ikiwa unapungukiwa nafasi ya uhifadhi, unaweza kutumia zana za Windows ili kuondoa folda hili. Ukweli ni kwamba, kama sehemu ya maboresho, Microsoft imeendelea kuongeza machaguo zaidi kwenye Mipangilio ya Windows (Windows Settings) ambayo yanaleta mfumo rafiki zaidi kwa watumiaji. Chaguo jipya katika Mipangilio linaloitwa “Storage sense” lina lengo la kukusaidia kupunguza vipengele na kuokoa ujazo wa uhifadhi (storage space). Pia inakuwezesha kufuta faili za muda mfupi (temporary files) na kuondoa folda ya Windows.old kwa kufuata hatua chache. Hivi ndivyo unavyoweza kufanya:

SOMA NA HII:  Marekani Inasema Korea ya Kaskazini Inahusika na Mashambulizi ya WannaCry

Kwa watumiaji wa Windows 10 na matoleo yanayofuatia.

Hatua 1. Nenda kwenye Settings, kisha chagua System.

Hatua 2. Kutoka kwenye orodha ya upande wa kushoto, chagua Storage.

Katika sehemu ya ‘Storage sense’ bonyeza sehemu iliyoandikwa  “Change how we free up space”


Hatua 3. Chini ya “Free up space now,” unaweza kuchagua kufuta folda la zamani la Windows.

Kisha bonyeza kitufe “Clean now.”

Hatua ya 4. Subiri Windows ikusanye mafaili na kuyafuta. Itaonyesha ujumbe itakapo maliza kufanya hivyo.
Kwenye SSD yangu ya 256GB, nimeongeza nafasi ya uhifadhi karibu 22GB.

Hatua ya 5. Storage sense ni kipengele kipya cha OS ambacho kwa kawaida huwa kimefungwa , lakini hapa utajifunza kazi zake na jinsi kinavyoweza kuwa na umuhimu kwako kwa kukuwezesha kufuta faili za muda mfupi, futa vitu kwenye recycle bin kila baada ya muda fulani, au hata faili kwenye folda ya Downloads. Uamuzi huu ni juu yako.

Njia mbadala ya uondoaji (inafanya kazi katika matoleo ya Windows yaliyopita)

Ikiwa unajaribu kufuta folda la Windows.old kwa kutumia njia ya kawaida ya File Explorer, OS itakuzuia kufanya hivyo kwa sababu inachukulia faili hizo kama sehemu ya faili za mfumo. Unaweza kupindua haya baada ya kubadilisha mipangilio ya vibali (permissions settings), lakini hakuna haja ya kufanya hivyo …

SOMA NA HII:  Fahamu Ukweli Kuhusu KeyBoards

Hatua ya 1. Nenda kwenye Start na  kisha andika ‘Disk Cleanup’.

Hatua ya 2. Kufungua Disk Cleanup na kuchagua system drive kuu.
Chombo hicho kitasanisha (scan) drive yako kuangalia faili zisizohitajika na data za zamani zilizohifadhiwa (old cached data). Hata hivyo, folda la Windows.old haitahesabiwa.

Hatua ya 3. Chagua chaguo  la “Clean up system files” . Chagua tena drive yako kuu na mchakato wa kuskani utafanyika tena.

Hatua ya 4. Matokeo ya scan yataonyesha aina tofauti za data, kutoka kwenye faili za Recycle Bin hadi kwenye cache za muda za mtandao. Wakati huu , “Temporary Windows installation files” zitakuwepo.

Hatua ya 5. Chagua faili zote unazotaka kuziondoa, ikiwa ni pamoja na faili za usanidi wa Windows (Windows installation files). Bofya OK. Kisha mapendekezo ya kuthibitisha yatafuata.

Ikiwa unatumia SSD ya kawaida, utafurahia kupata nafasi ya ziada.

Ikiwa unashangaa, ni salama kabisa kusafisha mafaili yaliyoorodheshwa na chombo hiki – usifute maudhui yaliyomo kwenye Recycle Bin ikiwa unataka kurejesha kitu baadaye (!). Vifaa vingine vya kusafisha kama CCleaner pia vinaweza kutumika ingawa katika kesi hii, si lazima.

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako