Jinsi Ya Kufuta Akaunti Yako Ya Facebook Moja Kwa Moja!


Unataka kujua jinsi ya kufuta akaunti yako ya Facebook? Katika mwongozo huu, tutakufundisha njia ya kufuta Facebook moja kwa moja, na kuelezea tofauti kati ya kusitisha kwa muda (Deactivate) na kufuta kabisa katika mtandao wa facebook.

Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kupelekea ukataka kufuta Facebook. Labda una wasiwasi juu ya faragha, labda unataka kupingana na maisha ya kisasa ya mitandao ya kijamii, au labda umechoshwa na mambo yanayoendelea mtandaoni. Kwa sababu yoyote ile, si vigumu sana kufuta kila kotu na kuishi maisha ya kuwa nje ya Facebook. Hapa ndivyo.

Kusitisha kwa muda (Deactivate) au Kufuta Facebook moja kwa moja – Kuna Tofauti gani?

Kuna njia mbili tofauti za kuiweka akaunti yako ya Facebook nje ya mtandao. Ya kwanza ni Kusitisha kwa muda (Deactivate), ambayo inamaanisha:

 • Unaweza kurejesha akaunti yako wakati wowote unavyotaka
 • Watu hawawezi kuona Facebook Timeline yako, au kukutafuta
 • Maelezo mengine yanaweza kuendelea kuonekana (kama ujumbe uliotuma)
 • Facebook inahifadhi maelezo ya akaunti yako (kama marafiki na maslahi) ikiwa unarudi tena

Lakini kufuta akaunti yako ni suala kubwa zaidi. Ikiwa utafuta akaunti yako:

 • Facebook huchelewa kufuta akaunti kwa siku chache baada ya ombi kufanywa. Ikiwa utaingia (log in) wakati wa kipindi hiki, basi kufuta akaunti kutasitishwa.
 •  Huwezi kurejesha upatikanaji wa akaunti yako ya Facebook mara tu baada ya kufutwa
 • Inaweza kuchukua hadi siku 90 kwa data zako zilizohifadhiwa katika mifumo ya ziada (backup systems ) ili kufutwa. Hata hivyo, maelezo yako hayapatikani kwenye Facebook ndani ya wakati huu.
 • Mambo mengine hayahifadhiwa katika akaunti yako, kama ujumbe uliowatumia marafiki – hizi zitabaki
 •  Nakala za nyenzo zingine (kama log records) zinaweza kubaki kwenye database za Facebook, lakini zipo “disassociated from personal identifiers,” kwa mujibu wa kampuni
Kimsingi, kusitisha Facebook kwa muda (Deactivate) ni kitendo cha kusimamisha akaunti kwa muda, wakati kufuta ni suluhisho la kudumu ambalo unapaswa kufikiria kwa makini kabla ya kuchagua.

JINSI YA KUSITISHA KWA MUDA (DEACTIVATE)

Kusitisha akaunti ya Facebook kwa muda (Deactivate), fuata hatua hizi:

 • Fungua akaunti yako ya facebook
 • Click katika menu (ile ya kuanguka chini iliyopo juu upande wa kulia)
 • Baada ya hapo ‘click’ Settings

 • Ukiwa katika Settings katika upande wa kushoto utaona Security bofya hapo
 • Sasa chagua “Deactivate Your Account” katika machaguo yaliyojitokeza

JINSI YA KUIPATA AKAUNTI ULIYOISITISHA KWA MUDA (DEACTIVATE)

Hii ni rahisi kabisa — Ingia facebook alafu ‘log in’ kwa kutumia taarifa zako ulizokuwa unazitumia kama kawaida. Moja kwa moja itafunguka akaunti yako na utaendelea kufurahia kutumia facebook.

JINSI YA KUFUTA AKAUNTI YA FACEBOOK MOJA KWA MOJA

Kufuta akaunti yako ya Facebook ni uamuzi mkubwa, hivyo hakikisha ni kitu ambacho unataka kufanya. Ikiwa unapenda au la, mitandao ya kijamii imeunganika katika jamii, na Facebook profile yako inaweza kuathiri urafiki, matarajio ya kazi, na fursa za kijamii. Zaidi, unaweza kukosa baadhi ya memes kwa kufuta Facebook, ni muhimu kwa vitu vingi, kama vile kuendelea kuwa karibu na marafiki kutoka nje na kuandaa matukio.

Ikiwa umeamua kufuta mtandao wa kijamii kwa manufaa binafsi, bofya “link” hii hapa chini na kisha chagua ‘Delete my account’ :

Kabla ya yote inashauriwa mtu kushusha (download) nakala ya taarifa zako za facebook. Kufanya Hivyo, Fuata Njia Hizi:

 • Fungua akaunti yako ya facebook
 • Click katika menu (ile ya kuanguka chini iliyopo juu upande wa kulia)
 • Kisha ‘click’ katika settiings
 • Katika “General” chagua “Download a copy of your Facebook data.” kwa ku’click’ hapo
 • Chagua ‘Start My Archive


Faili itakayo pakuliwa itakuwa na maelezo yako Facebook (Facebook profile information), kwa hiyo kuwa muangalifu sana kuhusu mahali unapoiweka.

Hapo utakuwa umefuta akaunti yako ya facebook moja kwa moja. Hii inamaanisha kuwa hutaweza kuitumia akaunti hiyo kamwe maana hii ni tofauti na kusitisha kwa mda (deactivate).

Je wewe ni mmoja kati ya wale wanaotaka kufuta akaunti zao za Facebook moja kwa moja na ulikua hujui njia za kufuata kufuta akaunti ya Facebook ? Tuambie kupitia sehemu yetu ya maoni.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA