Jinsi ya Kufungua Akaunti ya Paypal nchini Tanzania


Mediahuru imepokea barua pepe kutoka kwa wanachama wanataka kujua kama PayPal iko Tanzania na jinsi ya kujiunga na akaunti ya Paypal mtandaoni. Baadhi ya watu wanataka kufanya manunuzi ya mtandaoni lakini wengi wao wanashindwa kutokana na kutokua na vitu mbalimbali, moja ya vitu hivyo ambavyo tutangalia leo ni akaunti ya malipo ya paypal.

Paypal-Tanzania

PayPal ni jukwaa namba moja duniani la uhamisho wa fedha mtandaoni na hutumiwa na mamia ya mamilioni ya watu ulimwenguni kutuma na kupokea fedha. Paypal ina rahisisha malipo kati ya mununzi na muuzaji wa bidhaa au huduma flani kupitia kwenye mtandao. Kumiliki akaunti ya PayPal ni rahisi sana na unaweza kufanya hivyo kwa njia mbili.

Kama unataka kununua kitu kwenye mtandao mara nyingi unakutana na njia ya kulipia ya paypal hivyo kama huna akaunti hiyo inakuwa ni ngumu sana wewe kuweza kukamilisha manunuzi hayo, ndio maana leo tunakuletea hatua kwa hatua jinsi ya kujiunga na akaunti ya paypal.

Fuata hatua hizi kama zilivyo kwenye ukurasa huu ni muhimu kuzingatia kila hatua kama ilivyo:

  1. Jambo la kwanza unalotakiwa kufanya ni kwenda kwenye www.paypal.com/tz
  2. Bonyeza signup…chagua kibinafsi au biashara (personal or business)
  3. Binafsi itakuwa kwajili ya kadi yako ya debit ya kibinafsi (personal debit card) na biashara ni kwa kadi yako ya debit ya kampuni (ikiwa unayo). Ninashauri bonyeza “personal” ikiwa hii ni mara yako ya kwanza.
  4. Baada ya kuchagua “personal”, bofya kuendelea … unapaswa kuona “Tanzania” katika eneo la kushuka, anwani yako ya barua pepe na neno la siri.
  5. Jaza anwani yako ya barua pepe (haipaswi kuwa Gmail au yahoo. Inaweza kuwa @jinalakampuniyako)
  6. Andika katika eneo la neno lako la siri na uhakikishe kuwa unaweza kuikumbuka
  7. Nenda kwenye ukurasa unaofuata na ujaze maelezo mengine kama majina, tarehe ya kuzaliwa, anwani na nambari ya simu.
  8. Pia wakati wa kujaza anwani yako, hakikisha kuwa inafanana na maelezo sawa na anwani uliyoijaza wakati unafungua akaunti ya benki.
  9. Itakupeleka kwenye ukurasa ambapo utajaza maelezo yako ya kadi ya benk (debit card details)
  10. Andika namba yako ya kadi (card number), tarehe ya kumalizika (expiry date) na tarakimu tatu za mwisho zilizopo nyuma ya kadi yako ya benki.
  11. Nenda kwenye akaunti yako ya barua pepe na bofya kuthibitisha (verify)
  12. Voila!! Akaunti yako imekamilika !!
  13. Jaribu kwa kutuma $ 10 kwa mtu yeyote au akaunti yako ya PayPal nje ya nchi (ikiwa unayo)

Kumbuka kuwezesha Kadi yako ya Bank na Huduma ya Internet Banking ni lazima uwe na kadi ya bank (ATM Card)  kutoka bank yoyote yenye kutoa huduma za internet banking, hapa kumbuka nilazima kuomba huduma hii kuwezeshwa kwenye kadi yako sio kila kadi inayo huduma hii bali ni lazima kuomba huduma hii pamoja na kujaza fomu maalumu, bank nyingi hapa Tanzania zinafanya huduma hii bure kabisa hivyo ni rahisi kupata huduma hii.

Kwa mujibu wa PayPal, wakazi wa Tanzania ambao wana akaunti ya PayPal wanaweza kutuma fedha kwa mtu mwingine yeyote ambaye ana Akaunti ya PayPal lakini hawawezi kupokea pesa. Kipengele hiki kimefungwa nafikiri pengine ni kwa sababu ya sheria na kanuni za benki za kimataifa.

2 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

 1. Kwenye kujisajili na paypal ktka kuandika email umesema tusiandike yahoo au gmaili bali tuandike jina la kampuni sasa hilo jina la kampuni ndo lipi? Na kama huna kampuni je inakuaje ?

  1. Ndugu sio lazima uwe na email yenye jina la kampuni unaweza kutumia email yako ya gmail au yahoo (unashauriwa kutumia email binafsi kwa sababu za kiusalama zaidi.

ZINAZOHUSIANA