Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi Mtandaoni Ebay & Amazon na Kupokea Mzigo Kwa Tanzania


Ukuwaji wa sayansi na teknolojia imerahisisha mambo mengi katika jamii zetu na kuweza kutuletea ufanisi wa hali ya juu katika shughuli zetu za kila siku. Sasa unaweza kununua, kuuza bidhaa mbalimbali mtandaoni kulingana na mahali ulipo.

kufanya Manunuzi Mtandaoni

Unaweza kufanya manunuzi haya kupitia tovuti mbalimbali ambazo zinatoa huduma hii ya uuzaji na ununuaji wa bidhaa na huduma mbalimbali waweza sema ni soko huru la kimtandao. Inategemea wewe sasa unahitaji kutumia soko gani. Watu wengi  wanatamani kununua bidhaa kutoka kwenye maduka yaliyopo Marekani kama Amazon, Ebay, Best Buy, Walmart, Official stores za makampuni makubwa na mengine mengi ila hawajui wafanyeje.

Kuagiza bidhaa kwenye maduka ya mtandaoni yaliyopo marekani ni rahisi sana, kuna vitu vifuatwavyo vinahitajika.

 • Uelewa kuhusu usalama wa duka unalotaka kununua bidhaa.
 • Kuwa na Kadi ya benki iliyounganishwa na Visa au MasterCard.
 • Paypal account kwajili ya kufanya manunuzi mtandaoni
 • Kuwa na anuani ya marekani, kwa sababu sio maduka yote yanaweza kukutumia bidhaa au mzigo hadi Tanzania
 • Malipo ya Kodi Tanzania

Usalama wa duka unalotaka kununua

Hapa nadhani ndo watu wengi wanapoogopa. Ni kweli mtandaoni kuna utapeli, ila hili unaweza kulidhibiti kama ukipata bidhaa zako toka kwenye maduka makubwa na maarufu kama Amazon, ebay, walmart nk au kutoka kwenye maduka ya wazalishaji moja kwa moja kama Sony nk.

Ila kuna baadhi ya bidhaa hazipatikani katika maduka yenye umaarufu, hii haimaanishi kwamba hawaaminiki, sema hapa inabidi kujiridhisha binafsi kabla hujafanya manunuzi. Unaweza jiridhisha kwa kuwasiliana nao, kusoma reviews za watu wengine mtandaoni, nk.

Kuongezea usalama, nashauri malipo yapitie kwenye akaunti yako ya Paypal. Nitazungumzia jinsi ya kujiunga na huduma hii.

Jinsi ya kupata Visa/MasterCard Card

Ili uweze kufanya manunuzi online itabidi uwe na kadi ya benki iliyounganishwa na Visa au MasterCard systems. Visa na MasterCard ni mifumo ya malipo inayokuwezesha kutumia akaunti yako ya benki kufanya manunuzi katika nchi nyingi duniani.

Kadi ambazo zimeunganishwa na mifumo hii zinakuwa na nembo ya Visa au MasterCard kama zinavyoonyeshwa hapa chini.

Kadi hizi zinakuwa na card number yenye tarakimu 16 kwa mbele ya kadi, mwezi na mwaka wa kuexpire na CSC/CVV namba inakuwa na tarakimu 3 (hii ni kama password) hizo ndo utakazotumia kufanya malipo. Iweke kadi yako mahali salama na usimpe mtu hizi namba, maana zinatosha kufanya manunuzi.

Unapoomba kadi hii kutoka benki angalia inayokuwezesha kuweka US$ hii itakusaidia kutopata “exchange rates” mbaya wakati unanunua bidhaa mtandaoni, sababu bidhaa nyingi zinauzwa kwa dola. Kadi ambazo hazikuruhusu kuweka US$  yani za shilingi unaweza kuzitumia pia ila angalia ambayo haina makato makubwa sana wakati unanunua vitu.

Unaweza kutumia benki ya BancABC, CRDB au benki nyingine zinazotoa kadi zinazoweza fanya manunuzi mtandaoni.

Paypal Account kwajili ya Kufanya Manunuzi Mtandaoni

PayPal ni biashara ya kimataifa ya kieletroniki (e-commerce) ya kuruhusu malipo na uhamisho wa fedha kufanywa kupitia mtandao. Uhamisho wa fedha mtandaoni hutumiwa kama njia mbadala ya kielektroniki ya kufanya malipo na mifumo ya kawaida, kama vile hundi na maagizo ya fedha (checks and money orders).

PayPal ni mfumo, unaofanya malipo kwa wauzaji wa mtandaoni, tovuti za mnada, na watumiaji wengine wa kibiashara, ambapo kufungua na kutumia akaunti hii kwa “malipo” ni bure , ila pale unapoanza “pokea” malipo kuna kuwa na gharama kidogo kuendana na kiasi kilichopokelewa.

Paypal akaunti itakusaidia kulinda taarifa za MasterCard au Visa zisiibiwe, kila mara unapofanya malipo, utakuwa unalipia kwa Paypal akaunti na si kadi yako. Na mfano ikatatokea umelipia kitu afu haujakipata unaweza ripoti tatizo na Paypal watakusaidia kutatua.

Ingawa kuna baadhi ya maduka hayasapoti malipo ya Paypal, ila asilimia kubwa ya maduka yanasapoti na nakushauri kufanya manunuzi kwenye maduka yanayosapoti Paypal, maana ni rahisi kurudishiwa hela yako pale utakapokuwa na tatizo na muuzaji, na pia ni njia salama ya kupambana na matapeli wa mtandaoni.

Ukishafungua akaunti na Paypal utahitajika kuunganisha kadi yako ya Visa/MasterCard na Paypal akaunti yako.

Paypal watahitaji kukuchaji nadhani $1 kwenye kadi yako ambayo watakurudishia ili kuweza kuunganisha kadi yako na account yako ya Paypal. Na utahitajika kuwapa nambari fulani ambayo inahusiana na hayo malipo ya $1 kwa ajili ya kuhakiki taarifa zako na kukuwezesha kuanza kutumia kadi yako.

Usijali Paypal watakupa maelekezo yote. Hii namba inayohusishwa na malipo ya $1 utaipata ukiwauliza benki waliyokupa kadi au kama una “online bank account” ya kadi yako utaweza kuiona hii namba.

Bidhaa Uliyonunua Inafikaje Tanzania

Hii ni mojawapo ya changamoto ya kuagiza bidhaa mtandaoni kutoka Marekani ni kuwa maduka mengi hayasapoti utumaji wa mizigo nje ya Marekani.

Kununua kutoka Ebay au Amazon unachotakiwa kujua ni makampuni yanayoaminika ya usambazaji wa vitu. Yanakusaidia kufanya ununuzi bila mipaka. Mengi hufanya kazi kwa kukupa anwani ya kipekee ya U.S kutumika kama anwani yako ya usafirishaji wakati unanunua bidhaa yoyote kutoka kwenye duka la U.S mtandaoni.

Duka hutuma bidhaa yako kwenye anwani yako ya U.S; kampuni inapokea bidhaa hiyo na kukuletea Tanzania kwa ada ndogo.

Kuna makampuni mbalimbali ya usambazaji lakini moja la kuaminika ni MyUS.com au Shipito kampuni hizi zinatumiwa na watu wengi wa Tanzania.

Ila hii huduma sio bure pia sio gharama kubwa ukizingatia kama kitu unachoagiza kina umuhimu kwako.

Malipo ya Kodi Tanzania

Mizigo ukipokea kuna kodi utachajiwa. Hii kodi itategemea na thamani ya mzigo iliyoandikwa kwenye risiti. Kodi unayotakiwa kulipa inafikaga hadi 50% ya thamani ya mzigo.

Kwenye akaunti yako ya Shipito au MyUs kabla hujatuma mzigo kuna fomu ya “customs clearance” unajaza, hii fomu ndo inabidi “uijaze vizuri tumia ujanja” kupunguza kiasi cha kodi utakacholipa. Pia unaweza wapa Shipito special request waondoe zile risiti za bei za mzigo na kuacha hii customs clearance fomu tu.

Swala la kodi ni gumu inabidi uwe umejipanga nalo. Ni vizuri kutumia USPS ili uweze “negotiate” kodi pale unapoenda pokea mizigo yako kwenye ofisi za Posta.

Hitimisho

Kuagiza bidhaa mtandaoni kutoka Marekani si ngumu kama watu wanavyodhani, ila changamoto kubwa ni gharama za utumaji mizigo kwenda Tanzania na gharama za kodi.

Kama una swali lolote tuandikie comment yako hapo chini au kama unataka wasiliana na sisi tuandikia kupitia fomu ya  “Wasiliana Nasi

2 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

 1. nime soma hii thread ila bado main problem wengi wetu kwenye kujaza fomuza hizi company za kutoka US to TZ hua kuna sehemu ya kujaza zip code ambao utaratibu huo nchini naona bado haujawa sawa kidogo kwahiyo nilikua naomba mnujuze kuhusiana na hili au tuwekee full steps of doing this transaction…..

  1. Karibu sana ndugu Ahmed kwenye jukwaa hili, unaweza kusoma zaidi kuhusu biashara za mtandaoni kwa kubonyeza link hizi:

   1. Jinsi ya Kufungua Akaunti ya Paypal nchini Tanzania
   2. Biashara ya mtandao inafanyikaje? Malipo na Changamoto za usafirishaji bidhaa

   Makala hizi zinaweza kukupa ufahamu zaidi kuhusu biashara na manunuzi mtandaoni, na kuhusu ombi lako la kupata ufafanuzi zaidi kuhusu ZIP code endelea kuwa karibu na tovuti yetu kwani siku ya kesho tutaweka makala hiyo kama ulivyoomba

   Asante

ZINAZOHUSIANA