AndroidMaujanja

Jinsi ya Kufanya Backup Kwenye Simu ya Android au Tablet

Kuvunja au kupoteza simu yako au tablet kunaboa. Lakini kitu kinachoboa zaidi ni kupoteza data zote za thamani kwenye kifaa chako.

Kuwa smart na hakikisha unafanya Backup nakala ya vitu vyako vyote muhimu na faili. Kwa kufanya Backup, unaweza kurejesha data zako kwa urahisi kwenye kifaa kipya na kuzitumia wakati wowote.

Backup ya data kwenye simu yako ya Android au tablet ni rahisi. Ingawa kuna programu nyingi ambazo unaweza kupakua na kuziweka ambazo zitasaidia kurejesha data zako, hizi ni rahisi zaidi.

Kwa Kutumia Google

Njia rahisi na nyepesi ya kufanya back up kwenye simu yako ya Android ni kupitia Google kwa kutumia kipengele cha Android Backup Service ndani ya simu yako.

Ili kuifungua, nenda kwenye Settings > Backup & reset na hakikisha “Back up my data” imefunguka (turn on). Haya ni maelekezo kwa vifaa vya Google Nexus, lakini unaweza kupata mipangilio zaidi au chini ya hapa katika programu ya Mipangilio (Settings app)  kulingana na kifaa chako.

Kwa Huduma ya Android Backup, mipangilio ifuatayo itahifadhiwa kwenye Hifadhi ya Google – Google Driveya kwajili ya kurejesha baadaye: Google Calendar, mitandao ya Wi-Fi na nywila (passwords) zake, screen wallpapers, Gmail, apps zilizowekwa kupitia Google Play, mipangilio ya kuonyesha (display settings), lugha na mipangilio ya kuingiza (input settings), tarehe & Wakati, na mipangilio ya app zingine

SOMA NA HII:  Simujanja Unlocked: Maana ya Processor na Kazi Yake Kwenye Simu

Backup ya Samsung

Vifaa vya Samsung vinakuja na huduma yao ya backup. Ili kurejesha simu yako au tablet kupitia Samsung, unatakiwa kujiandikisha kwenye akaunti ya Samsung.

Mara baada ya kupata akaunti ya Samsung, nenda kwenye Settings > General > Backup and reset > Back up my data (chini ya akaunti ya Samsung) kisha ingia (log in).

Ndani, utaona chaguzi za kurejesha data kwajili Accessibility settings, Clock, Mawasiliano, Barua pepe , Ujumbe na Simu. Unaweza pia kutumia Auto Backup , ambayo huanza kazi saa moja baada ya ku-charge cha simu yako, unapounganishwa na Wi-Fi na skrini ikizimwa.

Manual backup

Ikiwa huuamini mfumo wa cloud kuhifadhi data zako, unaweza kurejesha tena faili zako njia kwa mtindo wa kizamani: hifadhi kwenye kompyuta yako.

Ili kuhamishia faili kama muziki, picha, video, na nyaraka kwenye kompyuta yako, kwanza uunganisha kifaa chako kwenye kompyuta kupitia cable ya microUSB au USB Type-C (kwa vifaa vipya). Kwenye Windows, kifaa chako cha Android kitaonyeshwa kama external drive na unatakiwa kufanya “drag and drop” tu ya faili unayotaka kuhamishia kwenye hard drive ya kompyuta yako.

Watumiaji wa Mac wanatakiwa kupakua na ku-install Android File Transfer kwenye Mac zao ili kutambua kifaa cha Android; Pia ni mchakato wa “drag-and-drop” faili kutoka Android hadi Mac.

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kuflash Simu za Tecno Kwa Kutumia SP Flash Tool

Kuhifadhi Picha

Jinsi ya Kufanya Backup Kwenye Simu ya Android au Tablet

Kuna njia zaidi ya 100 za kurejesha picha zako. Unaweza kutumia huduma yoyote ya bure au za kulipia za kama Google Drive, Microsoft OneDrive, Dropbox, Flickr, Box na Amazon Photos (kwajili ya Prime subscribers). Kila moja ina faida na hasara zake.

Tunayopenda ni Google Photos, ambayo inakuwezesha kuhifadhi picha kubwa bila kupunguzwa (hadi megapixels 16 kila mmoja) na video (hadi 1080p resolution).

Kufanya Back up ya picha zako zote kwenye Google Photos ni rahisi na unachotakiwa kufanya ni kupakua app hii kwenye kifaa chako na uiruhusu kupakia (upload) kila kitu kwenye mfumo wa cloud.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako