Jinsi ya Kudownload Youtube Videos kwa kutumia simu yako


Uwezo wa kuangalia video za youtube moja kwa moja kwenye simu zetu za smartphones ni moja ya vitu ambavyo watu wengi wanafurahia. Lakini wengi wetu tunatamani kuwa na baadhi ya video tunazozipenda kwenye simu ili tuweze kuzitazama tena na tena hata pale ambapo hatuna mawasiliano ya intaneti, hapa ndipo umuhimu wa kujua jinsi ya kudownload video hizi unapokuja.

Jinsi ya Kudownload Youtube Videos kwa kutumia simu yako-MEDIAHURU

Google hawaruhusu mtu kupakua (kudownload) video kutoka Youtube hivyo hakuna kitufe au link yoyote itakayokuwezesha kupakua video moja kwa moja. Lakini kwa msaada wa plugins na application hili linawezekana sasa, leo tutaangalia baadhi ya njia rahisi za kudownload video kutoka youtube.

Hatua Muhimu za Kufuata;

Haatua ya 1: Download Tubemate kutoka katika tovuti yao

Tubemate ni application ya bure inayokuwezesha kupakua video kutoka Youtube kwa urahisi zaidi na katika formats tofauti tofauti. Fungua kivinjari chako (web browser) na bonyeza hapa ili kuweza kupakua application hii kutoka katika tovuti yao. ni vizuri kupakua application hii kutoka katika tovuti yao kwa sababu kuna application nyingi feki zinazotumia jina hili katika playstore. Kuwa makini kuchagua link ya Android Freeware kama utaamua kwenda moja kwa moja kwenye website yao kwa kutumia adress ya tubemate.net.

Hatua ya 2: Inapoanza tu kudownlod simu yako itakupa ujumbe wa kukuonya kuwa faili unalojaribu kulidownoad linaweza kuharibu kifaa chako, usihofu android wameweka onyo hili kwa application zote utakazojaribu kudownload nje ya playstore. Baada ya kumaiza kudownload, funga hilo faili (hapa inategemea na kivinjari chako na sehemu uliyoset mafaili yote ya kupakua yahifadhiwe), litakuletea ujumbe wa kukataza kuinstall application nje ya google play, bonyeza “Go to settings” na washa au ruhusu kwa kuwasha kitufe cha “Unknown Sources”.

Hatua ya 3: Endelea na zoezi la kuinstall Tubemate kwa kupitia hatua chache mpaka pale itakapomaliza. Baada ya kumaliza fungua application yako kwa kubonyeza icon iliyotokea katika home screen yako au katika sehemu ya applications.

Step 4: Unaweza kufanya setting ya baadhi vitu kulingana na mahitaji yako, ila pale inapofunguka tu itakuletea orodha ya video kama ile ya youtube, unaweza ukatafuta video yoyote ile kutoka youtube hapo kwa kubonyeza eneo la kutafuta (search). Tafuta video unayotaka kuipakua, kwa juu utaona mshale wa kijani unaoelekea chini, bofya hapo na tubemate itakupa mifumo tofauti ya ubora wa video hivyo utachagua kulingana na mahitaji yako. Hapo kuna mpaka chaguo la MP3 kama utapenda kupakua audio, kisha bonyeza “Download” chini kabisa.

Hatua ya 5: Baada tu ya kubonyeza download tubmate itaanza kupakua video uliyoichagua, itakapomaliza utaiona katika notification area (uzi wa juu) na unaweza ukagusa hapo ili kuifungua na kuiangalia.

 

Ningependa kusikia kutoka kwako, Umejaribu kutumia njia hii ? Je, una swali lolote kuhusiana na tubemate? Tafadhali uliza swali lako kupitia sehemu ya maoni ili upate kujibiwa, usisite kushare hii kwa watu unaowapenda ili wajifunze kupakua video wanazozipenda bila tabu.

Kwa Habari Zaidi Na Maujanja Mbalimbali Ya Teknolojia Endelea Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa Mediahuru Kila Siku Kwani Daima Tunaaminika Katika Teknolojia!

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA