Jinsi ya kudownload picha na video kwenye status ya mtu WhatsApp


WhatsApp Status ilianzishwa rasmi mwaka 2017. Ni njia ambayo mtandao wa WhatsApp uliitumia kushindana na Snapchat, kwa baadhi ya watumiaji ulikuwa uboreshaji mkubwa lakini wengine hawaipendi. Mtandaoni watu wengi wamekuwa wakitafuta njia ya kusave / kudownload videos au picha za mtu kwenye status yake WhatsApp, lakini kabla ya kufika huko ni vyema tukafahamu matatizo 2 ambayo watu wengi wamekuwa wakiyalalamikia zaidi kuhusu whatsapp status.

kudownload

Matatizo 2 ya WhatsApp Status

Ndio, kipengele hiki ni kitu kinachovutia zaidi kwenye Whatsapp lakini kuna maeneo ambayo bado yanahitaji kuboresha kwenye WhatsApp status. Watumiaji wa WhatsApp wamekwenda mbali zaidi kwa kupakua App ya Android ambayo sio kutoka kwa Whatsapp kwa madhumuni pekee ya kutumia WhatsApp status. Watumiaji wengi wamelalamika juu ya haya:

  • Status Zinafutika Mara Moja.
  • Unapoangalia Status (Image) inaonyesha sekunde chache tu na ni vigumu kusoma maandishi yoyote kwenye picha.

Katika makala hii, nitakufundisha jinsi ya kusave Picha na Video za Whatsapp kwenye Whatsapp. Kutatua Zaidi ya 90% ya Vikwazo vya WhatsApp Status ikiwa siyo vyote. Ni rahisi sana na njia ya haraka ya kusave Whatsapp status na hakuna haja ya kupakua Application yoyote kwajili ya kufanya hivyo.

[irp]

Jinsi ya Kusave Picha au Video za Whatsapp Status

  1. Washa Intaneti na Fungua Akaunti yako ya Whatsapp
  2. Nenda kwenye Status kisha angalia status unayotaka kupakua / Ihifadhi
  3. Kisha fungua File Manager yako
  4. Nenda kwenye Settings na kisha Show Hidden Files
  5. Kisha nenda kwenye Folder: Whatsapp –> Media –> .statuses
  6. Huko unaweza kuona WhatsApp Status za watu wote
  7. Unachotakiwa kufanya ni Copy/Move Faili  kwenye folda nyingine
  8.  Ni hayo tu!!! Umepakua whatsapp status Video/Picha za rafiki zako.

Umepata matatizo / changamoto yoyote wakati wa mafunzo haya? Tafadhali tutumie ujumbe kwa kutumia sanduku la maoni hapa chini.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA