AppsIntaneti

Jinsi Ya Kuchukua Screenshot Bila Kutumia Kibonyezo Cha Kuzima Simu Kwenye Android

Screenshot ni njia rahisi sana ya kufikisha ujumbe kama ulivyo kwa mlengwa, maana ujumbe unaenda kama ulivyo bila ya kuongeza neno lolote. Kwa upande wako huwa unafanikiwa kupiga ‘screenshot’ kwa urahisi au ndio mpaka ubonyeze vibonyezo vingi kwa wakati mmoja?

Kama jibu ni ndio basi leo Mediahuru tunakuletea maujanja ya Screenshot bila ya kubonyeza vibonyezo vingi njia hii itakua mkombozi wako wa dhati.

FUATA HATUA HIZI:

Kwanza ingia katika soko la Google Play Store na kisha pakua App ya Screenshot Assistant

Baada ya kuishusha ukiifungua tuu kwa mara ya kwanza itakua inakupa maelezo kadhaa juu ya jinsi ya kuitumia. Baada ya hapo itakubidi ufanye maboresho kidogo kwa kuchagua App ambayo itakua katika mstari wa mbele katika kukupa msaada

Ukichagua Screenshot assistant kama kama App ya msaada (assistant) hutakua na uwezo wa kutumia Google kama App yako ya msaada kama ilivyokua mwanzo. ukimaliza uchaguzi huo kisha ‘Save’

Jinsi ya kupiga Screenshot’ ni rahisi sana kwani itakubidi ubonyezo kibonyezo cha ‘home’ (cha kurudia katika uso wa simu) kwa sekunde chache bila kuacha na kisha itajipiga

Kizuri kuhusiana na App hii ni kwamba ukishapiga hiyo Screen shot’ utapata machaguzi mengine kabambe kama vile ku’crop’ hiyo screenshot’ na mambo mengine mengi kama vile ku’share.

SOMA NA HII:  Twitter inajaribu Lite Android app

Baada ya hapo unaweza ukasave na ukaanza kuitumia wewe mwenyewe binafsi au ukawatumia watu uliokusudia.

Mpaka hapo utakua ushapata ujuzi sio? unaweza kutoa maoni yako pia kushirikisha njia zingine rahisi ambazo unazitumia kupiga screenshot.

Zinazohusiana

Toa Maoni Hapa:

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako