Jinsi ya kubuni neno la siri thabiti na kuweka taarifa zako salama.


Neno la siri ndio ulinzi wa kwanza dhidi ya wahalifu wa mtandaoni. Ni muhimu kuchagua maneno ya siri thabiti ambayo ni tofauti kwa kila akaunti zako muhimu na ni vizuri kusasisha neno lako la siri mara kwa mara. Fuata vidokezo hivi ili uunde neno la siri thabiti na uliweke salama.

Tumia neno la siri la kipekee kwa kila akaunti yako muhimu kama vile ya barua pepe na ya benki ya mtandaoni.

Kuchagua neno la siri sawa kwa kila akaunti yako mtandaoni ni sawa na kutumia ufunguo mmoja kufunga nyumba yako, gari na ofisi – mhalifu akifikia moja, zingine zote zitaathiriwa. Hivyo usitumie neno la siri sawa katika jarida la mtandaoni, akaunti yako ya barua pepe au benki. Inaweza kuwa kazi ngumu kiasi, lakini kuchagua maneno ya siri mengi hukuweka salama.

Weka neno lako la siri katika eneo la siri ambapo halitaonekani kwa urahisi.

Kuandika maneno ya siri si wazo baya. Lakini ukifanya hivvyo, usiache madaftari/karatasi yenye maneno yako ya siri mahali yanapoweza kuonekana kwa urahisi, kwenye kompyuta yako au mezani.

SOMA NA HII:  Jinsi ya kugundua (na kuepuka) barua pepe za udanganyifu

Tumia neno la siri refu linalojumuisha nambari, herufi na alama

Neno lako la siri likiwa refu, basi itakuwa vigumu kulikisia. Hivyo lifanye neno la siri kuwa refu ili ikusaidie kuweka taarifa zako salama. Kuongeza nambari, alama na mchanganyiko wa herufi kubwa na ndogo hufanya iwe vigumu zaidi kwa wanaotaka kuchungulia au wengine, kukisia au kujua neno lako la siri. Tafadhali usitumia ‘123456’ au ‘nenosiri,’ na pia jiepushe na kutumia maelezo yanayopatikana hadharani kama vile nambari yako ya simu, katika maneno yako ya siri. Si vizuri, wala si salama!

Jaribu kutumia fungu la maneno ambalo ni wewe tu unayelifahamu

Njia moja nzuri ni kufikiria fungu la maneno ambalo ni wewe pekee unayelijua, na ulihusishe na tovuti fulani kukusaidia kulikumbuka. Kwa barua pepe yako unaweza kuanza kwa “Rafiki yangu Tom hunitumia barua pepe ya kufurahisha mara moja kwa siku” na kisha utumie nambari na herufi ili kuliunda upya. “RayT;Hu&Bp:)” ni neno la siri lenye herufi tofauti. Kisha rudia utaratibu huu kwa tovuti zingine.

SOMA NA HII:  Mambo Yaliyompa Ushindi Mmiliki wa Facebook Dhidi ya Maseneta wa Marekani

Weka chaguo zako za kurejesha uwezo wa kutumia akaunti na uzisasishe

Ikiwa utasahau neno lako la siri au ushindwe kuingia kwenye akaunti, unahitaji njia ya kurudi kwenye akaunti yako. Huduma nyingi zitakutumia barua pepe katika anwani ya barua pepe ya kurejesha uwezo wa kufikia akaunti ikiwa unahitaji kuweka neno la siri jipya, hivyo hakikisha barua pepe yako ya urejeshi imesasishwa na bado unaweza kuifikia akaunti hiyo.

Wakati mwingine unaweza pia kuongeza nambari ya simu kwenye wasifu wako ili utumiwe msimbo wa kuweka neno la siri jipya kupitia SMS. Kuwa na nambari yako ya simu ya mkononi kwenye akaunti yako ni mojawapo ya njia rahisi na za kuaminika za kusaidia kuweka akaunti yako salama.

Kwa mfano, watoa huduma wanaweza kutumia nambari yako ya simu kutoa changamoto kwa wale wanaojaribu kuingia kwenye akaunti yako bila idhini, na kukutumia msimbo wa uthibitishaji ili uweze kuingia kwenye akaunti yako endapo utashindwa kuifikia.

SOMA NA HII:  Baada ya taarifa za Cambridge Analytica, Vyama vya upinzani nchini Kenya vinataka uchunguzi wa kampeni za uchaguzi

Simu yako ya mkononi ni mbinu salama zaidi ya kuthibitisha utambulisho kuliko anwani yako ya barua pepe ya urejeshi au swali la usalama kwa sababu, tofauti na mbinu hizo zingine mbili, una umiliki halisi wa simu yako ya mkononi.

Hata hivyo, ikiwa hutaki au huwezi kuongeza nambari ya simu kwenye akaunti yako, tovuti nyingi zinaweza kukuuliza uchague swali la kuthibitisha utambulisho wako endapo utasahau neno lako la siri. Ikiwa huduma unayotumia inakuruhusu ujitungie swali lako mwenyewe, jaribu kupata swali lenye jibu ambalo ni wewe pekee unayelijua na si kitu ambacho umechapisha hadharani au umeshiriki kwenye mitandao jamii.

Jaribu kupata njia ya kufanya swali liwe la kipekee lakini rahisi kukumbuka – unaweza kufanya hivi kwa kutumia kidokezo kilicho hapo juu – ili hata mtu akijaribu kukisia jibu, hatajua jinsi ya kulijaza sawa sawa. Ni muhimu sana kwako kukumbuka jibu hili – ukilisahau huenda usiweze tena kuingia kwenye akaunti yako.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *