Jinsi ya Kubadili neno la siri (Password) kwenye Windows 7


Kubadilisha neno la siri (password) kwenye Windows 7 mara kwa mara ni tabia nzuri ya kukusaidia kuweka PC yako salama. Unaweza pia kutaka kubadilisha password yako ya Windows 7 ikiwa unapata shida kukumbuka au kutumia ya sasa.

Jinsi ya Kubadili neno la siri (Password) kwenye Windows 7-mediahuru

Kubadilisha nenola siri kwenye Windows 7 ni rahisi sana. Fuata hatua zilizo hapa chini ili kubadilisha password yako ya Windows 7:

Kumbuka: Ikiwa unajaribu kubadili neno lako la siri kwenye Windows 7 kwa sababu umeiisahau na hauwezi tena kutumia Windows, angalia hatua nambari # 2 chini ya ukurasa kwa msaada zaidi.

Kubadilisha Neno la siri kwenye Windows 7 yako ni rahisi

Mabadiliko kawaida huchukua chini ya dakika chache. Hapa ni jinsi ya kufanya hivyo.

  1. Bofya kwenye Start na kish Control Panel.
  2. Bonya kwenye link ya User Accounts and Family Safety.Kumbuka: Ikiwa unatazama Large icons au Small icons ya Control Panel, hutaona kiungo(link) hii. Bonyeza tu icon ya User Accounts na endelee na hatua ya 4.
  3. Bofya kwenye link ya User Accounts.
  4. Katika Make changes to your user account kwenye eneo la User Accounts window, bofya link ya Change your password.
  5. Katika sanduku la kwanza la maandishi, ingiza neno lako la siri la sasa.
  6. Katika masanduku mawili ya maandishi yanayofata, ingiza neno la siri ambalo ungependa kuanza kulitumia.Kuingiza neno la siri mara mbili husaidia kuhakikisha kuwa umeandika neno la siri kwa usahihi.
  7. Katika sanduku la maandishi la mwisho, unatakiwa Uandike kidokezo cha neno la siri (Type a password hint). Hatua hii ni chaguo sio lazima lakini mimi hupendekeza sana kuitumia. Ikiwa unajaribu kuingia kwenye Windows 7 lakini  neno la siri uliloingiza likawa sio sahihi, hint hii itaonyeshwa, ambayo kwa matumaini yangu itarudisha kumbukumbu zako.
  8. Bofya kwenye button ya Change password ili kuthibitisha mabadiliko yako.
  9. Sasa unaweza kufunga User Accounts window.
  10. Sasa neno lako la siri kwenye Windows 7 limebadilishwa, hapa lazima utumie neno la siri jipya ili uingie kwenye Windows 7 kwanzia sasa.
  11. Unda Windows 7 password reset disk. Ingawa si sehemu inayohitajika ya kubadilisha neno lako la siri, mimi hupendekeza sana kufanya hivyo. Kumbuka: Huna haja ya kuunda upya password reset disk mpya ikiwa tayari unayo. Password reset disk ya awali itafanya kazi bila kujali mara ngapi unabadilisha password yako ya Windows 7.
   Tips:
  1. Wewe sio mtumiaji wa Windows 7? Soma Jinsi ya Kubadili neno la siri (Password) katika Windows? kwajili ya maelezo maalumu kwa toleo lako la Windows.
  2. Kama unataka kubadilisha neno la siri kwenye Windows 7 kwa sababu umesahau neno la siri la awalizi kutumia/kuingia kwenye  Windows basi huwezi kutumia njia iliyoelezewa hapo juu.Ila unaweza kutumia programu ya Windows password recovery ya bure kutoa au kureset neno la siri hata kama huwezi kuingia kwenye Windows 7 kabisa. Unaweza kubadilisha neno la siri kwa kutumia maelezo hayo hapo juu.Chaguzi nyingine zipo pia. Angalia Msaada! Nimesahau neno la siri (password) yangu ya Windows 7! Kwa mawazo mengine zaidi.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA