AndroidMaujanja

Jinsi ya Ku “Reset” Simu Yako ya Andriod – Njia 2 Zinazofanya Kazi

Ikiwa hupendezewi na mwenendo wa simu yako, unalalamika kila dakika simu inachukua zaidi ya dakika 10 kufungua app, ni muda wa kufanya factory reset. Factory reset itafuta data zote za simu yako na kuirejesha kwenye mipangilio ambayo huja na simu. Kabla ya kutupa simu yako kwenye takataka, angalia mwongozo huu.

Njia ya kwanza: Kureset Kwa Kutumia Factory Reset

  • Nenda kwenye Menu ya simu yako kisha unaenda kwenye Settings.
  • Kisha unabofya Backup And Restore baada ya hapo unaenda kwenye Factory Reset.

Hapa ni muhimu kujua kwamba ukifanya hivi vitu vyako vitafutika hivyo ni muhimu kufanya back up ya data zako zote kabla hujafanya hivi.

  • Bofya “Reset Device” ili uondoe data zote na kurejesha mipangilio ya kiwanda. Kwa kawaida, hifadhi ya ndani ya simu yako yote itafutwa.

Kumbuka: – Ikiwa unataka kufuta data zote kwenye memori kadi ya simu yako pia, weka alama ya tiki kwenye sanduku chini ya skrini.

  • Hakikisha mchakato kwa kuchagua “Erase Everything“. Hii itafuta data zote na kurejea kwenye mipangilio ya kiwanda ya kifaa chako. Simu yako itakuwa kama mpya yani ndio inatumika kwa mara ya kwanza.

Njia ya Pili: Kureset kwa kutumia System Restore

Hi njia ni ngumu kidogo na haifahamiki sana lakini ndio njia yenye nguvu. Sifa za njia hii ni kwamba inafanya kazi hata simu yako ikiwa imeji ‘lock’ (kama umesahau pattern au password ya simu yako).

SOMA NA HII:  Jinsi ya kuweka pesa kwenye akaunti yangu ya SportPesa

1.Kwanza zima simu yako ya Android

      • Kama ni Mtumiaji Wa Samsung Bonyeza: Sauti juu + Home + Kuzima. Mara baada ya simu kunguruma achia kitufe cha kuzima. Mara simu ikiwa katika modi ya ‘Recovery’ achia kitufe cha sauti juu na cha home pia
      • Kama Ni Mtumiaji Wa HTC Bonyeza: Sauti Chini + Kuzima. Simu ikiwa inawaka achia kitufe cha kuwasha, ukiona imetokea modi ya ‘Recovery’ achia kitufe cha Sauti Chini

2.Ukishaingia katika menyu ya System Restore tumia kitufe cha Sauti Juu Na Sauti Chini Kuchagua chaguo lako na kitufe cha kuwasha/kuzima simu kuchagua chaguo hilo

3. Sasa chagua chaguo lako kureset simu yako ya Android

Njia hii itachukua mda kidogo katika ufanyaji kazi wake laki unashauriwa kutotoa betri ya simu yako maana italeta hitilafu wakati wa kureset .

Naimani njia hizi zitakusaidia sana kureset simu yako mwenyewe bila kuwapelekea mafundi.  Toa maoni yako.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako