Jinsi Unavyoweza kutumia WhatsApp kwenye Kompyuta yako


Bila shaka intaneti imejaa programu nyingi za ujumbe wa papo hapo (instant messaging apps). Hata hivyo, hakuna hata moja ambayo imeweza kuzidi uwezo wa programu inayomilikiwa na Facebook. Ndio, tunazungumzia Whatsapp. Ilianza kufanya kazi rasmi mwaka 2009, imekusanya mabilioni ya watumiaji duniani kote mpaka sasa na inaonekana kama programu muhimu kwa watumiaji wengi. Kwa mwonekano wake rafiki kwa mtumiaji (user-friendly interface), utumaji wa ujumbe wa haraka, iwe ni maandishi, sauti, au video, Whatsapp haijawahi kushindwa kuvutia watumiaji wengine wengi zaidi kwa kuanzisha vipengele vipya kadhaa kila mara.

Kwa miaka michache, watumiaji wamekuwa wakitumia programu hii kwenye simu zao za mkononi na vifaa vngine vya mkononi. Hata hivyo, Whatsapp haijazuia kuitumia kwenye kompyuta. Lakini watumiaji wengi hawajui kwamba unaweza kuitumia kwenye kompyuta pia. Ikiwa bado hujui kwamba inafanya kazi vizuri sana kwenye kompyuta basi tuko hapa kukuambia jinsi ya kufanya hivyo.

Jaribu Toleo la Kompyuta!

Kwa wale ambao wamechoka kutumia programu hii kwenye simu zao na wanapaswa kuangalia simu janja zao kila mara kujua kama kuna ujumbe mpya hatimaye wanaweza kuwa nayo kwenye kompyuta zao hasa wakati wa kazi. Kuna njia mbili za kutumia programu hii kwenye kompyuta yako. Kwanza, inaweza kutumika kupitia WhatsApp Web kwenye kivinjari chako lakini tatizo la chaguo hili ni kwamba unatakiwa kufungua ukurasa wa wavuti na kuingia kila wakati unapofungua kivinjari. Chaguo jingine, rahisi zaidi, linahusisha wewe kupakua WhatsApp app kwa ajili ya Windows au Mac.

Jinsi ya kutumia Whatsapp kwenye Kompyuta

Hizi ni hatua za jinsi ya kutumia watsApp kwenye kompyuta yako.

Hatua ya 1:

Fungua link hii kupakua WhatsApp app kwenye kompyuta yako.

Hatua ya 2:

Baada ya kukamilisha mchakato wa kupakua (installation ), fungua programu kwenye kompyuta yako. Mara baada ya programu kufunguka, utaona skrini ya mwanzo ya kawaida ambayo ni sawa na ile ya WhatsApp Web..

Hatua ya 3:

Scan QR code kama unavyofanya kwajiri ya WhatsApp Web na kisha utakuwa tayari una uwezo wa kuitumia kwenye kompyuta yako.

Kidokezo: Ikiwa unataka kuhakikisha uhamisho thabiti wa ujumbe kwenye Whatsapp, basi inashauriwa kuunganisha kompyuta na simu janja yako kwenye mtandao sawa.

Unaweza kubadilisha picha yako ya wasifu, phone status na pia kupata mipangilio ya programu na taarifa (notifications) kwenye kompyuta kama vile unavyofanya kwenye programu ya simu.

Mchakato wa kupata Whatsapp kwenye kompyuta yako ni rahisi kama inavyoonekana! Kwa hiyo, unasubiri nini? Pata programu bora ya ujumbe wa papo hapo kwenye kompyuta yako sasa!

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA