Sambaza:

Nashusha video kutoka kwenye Facebook na kuzihifadhi kwenye Kompyuta yangu bila ya kutumia programu yoyote ile. Ki ukweli, video zinakuwa na ubora uleule baada ya kuzishusha kwenye komputer yangu. Natumia njia mbili kupakua video za Facebook na hapa nitakushirikisha na wewe uzijue njia hizi.

NJIA YA KWANZA

Tafuta video unataka kupakua – kisha bonyeza juu yake kuicheza/play.

Right click juu yake wakati unaicheza/play na kisha bonyeza “show video URL”

Ikifunguka utaona “video URL”. Tumia CTRL C kwenye keyboard yako kucopy URL

Tumia CTRL V kupaste video URL kwenye address bar ya browser yako

SOMA NA HII:  Mambo 5 Usiyoyajua Kuhusu Mtandao wa Instagram

Rekebisha URL ya video, toa neno “www” mwanzoni mwa URL kwa kuandika neno “m” (mfano: “https: // www” na “https: // m”) na kisha bonyeza Enter.

Kwa mfano, kama URL ya video ni :

https://www..facebook.com/netdivoepinmanager/videos/273371716398493/

Mimi naibadilisha https://www w na “m”, kama hivi:

https://m.facebook.com/netdivoepinmanager/videos/273371716398493/

Sasa baada ya kugonga “Enter” kwenye kibodi yako, utaona mwonekano wa mkononi (mobile view) , ambao hujaza screen nzima, kama hivi:

Hapa unachotakiwa kufanya ni kuicheza video, kisha right click kwenye video hiyo na chagua “Save video as” kama inavyoonekana hapo juu.

Kisha utaona chaguo la MP4. Chagua jina la faili na hifadhi kwenye kompyuta yako.

SOMA NA HII:  Jinsi ya kupata pesa au faida kwa kumiliki website au blogu

Ni rahisi hivyo.

NJIA YA PILI

Hii itakuwezesha wewe kudownload video za Facebook katika mfumo wa HD i.e ubora wa video unabaki vilevile

Nenda kwenye http://www.video-fb.com/

Kisha paste video URL yako kwenye sanduku na bonyeza “Get Link”

Bonyeza “download’ na hifadhi Facebook video kwenye PC yako

Ni hayo tu.

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako