Jinsi Data Zinavyohifadhiwa kwenye Diski Kuu na Umuhimu wa Kufanya Defragmentation


Kwanini  Defragmentation Inasaidia:  Vitu vyako vimehifadhiwa kwenye diski kuu (hard drive) katika namna ya mstari. Kwa lugha rahisi, hebu tuseme data zimehifadhiwa kwenye diski kuu kwenye mstari mmoja baada ya mwingine.

Defragmentation
Jinsi ya kufanya defragment ya diski kuu kwenye Window

Ikiwa unahariri (edit) faili moja na likapungua ukubwa wake, basi nafasi tupu itatengenezwa sehemu ilipoondolewa data iliyokuwepo.

Sasa ikiwa unajaribu kuhifadhi faili jingine, sehemu ya faili hilo itahifadhiwa katika nafasi iliyotengenezwa ambapo data ya awali ilikuwepo. Kiwango kidogo kilichobaki sasa kitahifadhiwa kwenye mstari unaofuata.

Hii inapelekea sehemu tofauti za faili kuhifadhiwa katika sehemu tofauti za diski kuu. Kwa maneno mengine, zinakuwa kwenye mgawanyiko (fragmented).

Tatizo hapa ni kuwa diski kuu inatakiwa kufanya kazi ngumu na kuchukua muda mrefu kufikia faili iliyohifadhiwa kwenye sehemu mbalimbali zilizogawanyika katika sehemu tofauti.

Defragmentation imewekwa kutatua tatizo hili kwa kuleta pamoja sehemu tofauti za faili na kuzifanya ziwe kwenye mpangilio unaofaa. Hii inafanya kufikia faili na kulifungua kwa kasi zaidi kuliko wakati imegawanyika.

Ili kuwezesha defragmentation kwenye Windows PC fanya hivi:

  1. Fungua Explorer, My Computer au This PC kuona vifaa vya uhifadhi (storage devices)
  2. Right click diski kuu (hard drive) na kisha chagua Properties
  3. Bofya kwenye Tools .
  4. Bonyeza Optimise chini ya Optimise and defragment drive
SOMA NA HII:  Jinsi ya kuongeza kasi ya simu yako ya Android

Muda utakao tumika kufanya defragmentation inategemea na ukubwa wa diski kuu yako na ni kiasi gani faili zimegawanyika.

2 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *