Apps za SimuIntaneti

Jihadhari na Programu Unayopakua kwenye Google Play.

Taarifa kutoka mitaani zinasema kuna programu kadhaa zisizofaa zimeweza kupita kwenye ulinzi wa Google.

Inashangaza kama inavyoonekana, ni kweli!

Licha ya ukweli kwamba Google inachunguza kila programu ili kuhakikisha kuwa hakuna “malicious” yoyote inayofaniki kuingia kwenye huduma yake ya Google Play , programu kadhaa zisizofaa zimefanikiwa. Mfano ni SMSVoca, programu inayochunguza maeneo wanayotoka watumiaji. Ilikuwa tayari imepata downloads milioni 1 kabla ya Google kuiondoa. Kisha kuna “malware Judy”, ambazo zimeambukiza programu zaidi ya 41 kwenye Duka la Google Play.

Ukweli wa kushangaza ni kwamba karibu programu 100 za aina hii zenye downloads zaidi ya milioni 1 zimepatikana hadi sasa (lakini sio na Google).

Zahivi karibuni ni Magic Browser na Noise detector ambazo kuna taarifa ya kuwa zina Ztorg malware , zinaweza ku-root smartphone bila idhini ya mtumiaji na pia kudhibiti huduma za SMS kwenye simu. Programu hizi zimepakuliwa zaidi ya mara 50,000 kabla ya kuondolewa kwa Google. Kwa hiyo, kama una programu hizi kwenye simu yako — Magic browser na Noise detector – unapaswa kuzifuta mara moja!

Je! Unaweza kufanya nini kujikinga?

Hakikisha unaangalia vibali vya programu kwa uangalifu na kufuatilia zile zinazoomba idhini isiyofaa. Pia, jaribu kusoma mapitio kabla ya kupakua.

Weka simu zako salama, Ndugu!

SOMA NA HII:  Error 505: Tatizo la kushindwa kupakua apps kutoka Google Play Store
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako