AndroidApps za SimuDownload

Je,Umejaribu Prisma App kwenye Android na iOS?

Ikiwa na zaidi ya downloads milioni 10 kwenye iOS store ndani ya wiki chache tangu uzinduzi wake, Prisma, programu ya filter iliyozinduliwa na programa wa Urusi ndani ya muda mfupi imekuwa programu ya picha maarufu. Ni, kitu gani maalum kuhusu app hii?

Tofauti na programu nyingine zinazotoa huduma kama hii, Prisma inatumia “cloud-based machine learning” kugeuza picha zako zisizo na mvuto kuwa mchoro wenye mvuto. Kwa hiyo, badala ya kutumia filter ambazo zinajenga overlay, Prisma inatumia akili ya ziada kujenga picha yako upya kutoka mwanzo.

Hata hivyo, kwa vile hii ni programu ya mtandaoni ambayo inahitaji kuunganishwa na intaneti, mimi nimegundua kuwa ilichukua sekunde 4 au zaidi kuwezesha kila filter ambayo si mbaya ukilinganisha na matokeo ya mwisho.

Kama bado hujaijaribu, acha kuwa wa mwaka 2015, unaweza kuijaribu?

Kuishusha (download) Bonyeza hapa kwa Android, au kwajili ya iOS

SOMA NA HII:  Dalai Lama azindua app ya bure kwajili ya watumiaji wa iPhone
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako