Home Nyingine Jeshi la Polisi lapiga marufuku mikusanyika vituo vya polisi

Jeshi la Polisi lapiga marufuku mikusanyika vituo vya polisi

0
0

Msemaji wa Jeshi la Polisi ACP Bulimba ametoa agizo la kuzuia ukusanyikaji wa waandishi pamoja na wananchi watu katika vituo vya polisi pindi watuhumiwa wakiitwa kuhojiwa.

Agizo hili linaanza kutekelezwa mara moja katika vituo vyote vya Jeshi la Polisi Tanzania bara na visiwani.

Kufuatia agizo hili la polisi, lililotolewa 14/02/2017 na Makao Makuu ya Polisi, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaokiuka agizo hilo.

Taarifa hii inakuja siku kadhaa baada ya Rais Magufuli kukemea hali ya wanakwaya wa kanisa la Ufufuo na Uzima kukusanyika na kuimba mapambio wakati wakimsubiri Askofu wa kanisa lao akihojiwa kwa tuhuma za madawa ya kulevya , huku wafuasi waliokuwa wamevalia sare za klabu ya Yanga, nao wakikusanyika na kusubiri mustakabali wa kiongozi wa klabu yao.

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *