Sambaza:

Miaka michache iliyopita katika mji wa Mbeya Mjini, nilikutana na Neema, msichana mwenye umri wa miaka 18. Neema alinishirikisha jinsi alivyokuwa na shauku juu ya teknolojia lakini alikuwa ameonywa sana na wazazi wake kwamba Wahandisi (Engineers) wanawake hawana nafasi. Baada ya uchunguzi zaidi, aliniambia kwamba anadhani ni kweli kwa sababu hakuna mifano mingi ya kuigwa (role models).

mazingira ya teknolojia ya Tanzania

Swala la kufikiria kwamba kazi ngumu zaidi ya kukamilisha theorem kamili kwajili ya zoezi la kutua mwezini ilifanywa na Katherine Johnson halikuwepo kabisa wakati hotuba ya Neil Armstrong iliyoelezea “hatua chache” imekuwa mantra ya safari ya anga za juu. Ni hivi karibuni tu ndio movie “Hidden figures” iliyotengenezwa kwa heshima ya Katherine Johnson imetolewa. Hii huleta tofauti kati ya mwanamume na mwanamke na hasa hasa, kupungua kwa wanawake katika sekta ya Teknolojia nchini Tanzania. Kwa madhumuni ya uelewa wa wazi, kutowathamini wanawake kuna sababisha ndoto nyingi kufa bila ya kufanyiwa kazi

Kudidimizwa kwa wanawake kunaweza kufanywa kwa aina tofauti; ya kikatili zaidi ni kudidimizwa na mfumo, ambapo kwa kawaida huwekwa katika ufahamu wa msichana mdogo nchini Tanzania kwamba teknolojia sio kwajili yao.

SOMA NA HII:  Facebook kufanya utafiti ili kuboresha habari zake

Uchunguzi Binafsi

Kwa uchunguzi wa kina nilioufanya nimegundua kushuka kwa Idadi ya wanawake wanaosoma masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM).  Baadhi ya mambo ninayohisi yamechangia kutokea kwa tatizo hili ni jukumu la wanawake kama walezi wa familia. Ukweli kwamba hawana mifano ya kuigwa, changamoto za kibaolojia na changamoto zingine za kazi kama “hatari” inayohusishwa na kazi za kiteknolojia. Kwa mfano, idadi ya wanawake wanasayansi wa kijiolojia imeshuka kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania ikilinganishwa na wanaume katika vyuo vikuu vya Tanzania kama inavyoelezwa na majarida mbalimbali.

Kwa Tanzania kufikia hatua muhimu za maendeleo katika vigezo na malengo mbalimbali ya maendeleo endelevu yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa, lazima kuwe na majadiliano ya haraka kuhusu suala hili.

Wanawake Mashujaa

Mbali na yote haya, ni lazima niseme baadhi ya wanawake wameamua kuthubutu na wanawake hawa wanaitwa mashujaa. Ninapozungumza ninahisi roho ya ‘uthubutu’ wa kufanya yasiyowezekani ndani yao. Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Joyce Ndalichako, Naibu Waziri wa zamani wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Eng. Stella Manyanya, Mwamvita Makamba kutoka Vodacom na nk, ni mifano michache ambayo mara moja imekuja akilini.

SOMA NA HII:  TAARIFA YA MKUTANO JUU YA MAPENDEKEZO YA VIWANGO VYA GHARAMA ZA MAINGILIANO YA MITANDAO YA SIMU NCHINI.

Wakati ninafurahi kuwa orodha ya wanawake mashujaa inaongezeka kwa haraka nchini Tanzania, bado naamini wanawake wanadidimizwa. Msingi wa hili ni uwiano wa wanawake na wanaume katika masuala ya teknolojia nchini. Je, kuna uwiano gani kati ya wanawake na wanaume maprogrammer ? Ni kampuni ngapi za teknolojia zinamilikiwa na wanawake?

Wauaji wengine wa Kimya Kimya

Ni jambo la kusikitisha kwamba wakati tunamulika zaidi juu ya Silicon Valley ya Marekani na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia huko Hollywood, tunasahau kwamba kuna unyanyasaji mwingi wa kijinsia dhidi ya wanawake katika maeneo ya Tanzania. Msichana mdogo, mwenye umbo la kuvutia sana ambaye ni mtaalumu wa teknolojia aliwahi kuniambia kuwa mikutano mingi hasa ya kuomba kazi hugeuka kuwa “kikao cha kugusa” na analazimika kuondoka eneo hilo. Aliendelea kwa kumtaja mwekezaji mmoja akisema “atapata fedha nyingi zaidi kuwa mchepuko wake kuliko kufanya mambo ya coding.” Hii inafanya idadi ya wanawake wanaoingia kwenye teknolojia kuwa ndogo sana.

SOMA NA HII:  Taarifa kutoka TANESCO kuhusu mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya LUKU

Kuingilia kati

Bila shaka, kuingilia kati sana kunazidi kuwahamasisha wanawake katika teknolojia; kuanzishwa kwa jamii kama ushirikiano wa wanawake katika Usimamizi na Biashara na mashirikisho mengine ya wanawake, naamini makundi haya na zaidi yanahitajika ili kuonyesha umuhimu wa wanawake katika sekta hii hasa ukizingatia kwamba wanawake wana ujuzi zaidi wa teknolojia.

Njia ya kwenda mbele

Njia moja ya sisi kusonga mbele ni kujifunza kupitia nchi washirika kama China ambayo hutoa uwiano wa nafasi katika makampuni ya teknolojia. Pia, masuala ya haki za wanawake yanapaswa kupitiwa upya na kuwe na nia ya serikali ya kuhamasisha wanawake katika teknolojia. Katika nchi ya Burkina Faso hivi sasa, wanawake wanaheshimiwa sana kwa sababu Thomas Sankara alisisitiza haki za wanawake na alitangaza siku ambazo wanaume na wanawake hubadilisha majukumu ili kuhakikisha kwamba mwanaume anajua vile mwanamke “avyojisikia”.

Kwa kweli, maadili ya kijamii yanapaswa kupitiwa upya kama njia ya kuzuia mwenendo huu.

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako