Habari za Teknolojia

JE, WAJUA: Ni njia gani zilizotumiwa kuhifadhi samaki zamani?

Kwa muda mrefu, samaki wamekuwa chakula muhimu.Tangu miaka ya zamani jamii mbalimbali zilijihusisha na uvuvi baadhi ya samaki waliowavua walitayarishwa kwenye “viwanda” vidogo vilivyokuwa karibu.


Mchoro unaoonyesha wavuvi wa kale wamisri

Mbinu ya kuhifadhi samaki ambayo huenda ilitumiwa na wavuvi zamani bado inatumiwa katika baadhi ya maeneo.

Kwanza, samaki hutolewa matumbo na kuoshwa kwa maji. Kitabu Studies in Ancient Technology kinaelezea hatua zinazofuata:

“Chumvi hupakwa kwenye mapezi, mdomo na magamba. Samaki waliotiwa chumvi kwa wingi hufunikwa kwa jamvi. Baada ya kuachwa kwa siku 3-5 rundo hilo hugeuzwa na kukaa tena kwa kipindi kama hicho. Wanapokaushwa kwa njia hiyo, umajimaji wa mwili hukauka na chumvi huingia ndani ya samaki. Baada ya kukauka, wanakuwa wagumu.”

Haijulikani samaki wangehifadhiwa kwa muda gani kupitia njia hiyo. Hata hivyo, kwa kuwa Wamisri wa kale waliuza samaki waliokaushwa huko Siria, hilo linaonyesha kwamba njia hizo zilifaulu.

SOMA NA HII:  Ifahamu Timu ya Mwitikio wa Kukabili Majanga ya Kompyuta Tanzania TZ-CERT

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako