Habari za Teknolojia

JE, WAJUA: Mafundi wa meli wa zamani walifanyaje ili vyombo vya baharini visiingie maji ?

Je wajua mafundi wa meli wa zamani walivyofanya ili kuzuia maji yasiingie ndani ya meli.?

Kwa kawaida walipaka lami kwenye nafasi kati ya mbao au hata upande wote wa nje, na pia upande wa ndani wa mashua au meli. Miaka mingi iliyopita Waroma, na jamii zingine walipaka lami kwenye mashua na meli zao ili kuzuia maji.

Lami iliyoyeyuka

Lami ilipatikana kwa wingi katika maeneo ambayo meli zilitengenezwa.

Lami asilia hupatikana katika hali mbili—ikiwa kavu au iliyoyeyuka. Mafundi wa meli wa zamani walitumia lami iliyoyeyuka; waliipaka moja kwa moja kwenye meli au mashua zao. Baada ya kupakwa, lami hiyo ilikauka na kuwa tabaka gumu lililozuia maji kuingia.

Katika vitabu vya dini kama Biblia lami ilipatikana kwenye nchi Tambarare ya Sidimu, iliyokuwa kwenye Bahari ya Chumvi, “ilikuwa imejaa mashimo ya lami.”—Mwanzo 14:10.

SOMA NA HII:  Hii ndio Teknolojia ya kutambua' wapenzi wa jinsia moja

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.