Elimu

Je Ni Kweli Walimu Hawana Thamani ?

Ukikaa karibu na walimu wengi , wanalalamika hawapewi thamani inayohitajika wanadai wanafanya kazi kubwa lakini mshahara ni mdogo, wengine wanasema hawapati muda wa ziada kufanya kazi zingine ili kujiongezea kipato pia makato ni mengi sana na hawapati stahiki zao kwa wakati.

Nikianza kuandika mambo magumu ambayo walimu wanadai kukumbana nayo nitajaza huu ukurasa, kwa ufupi tu:
1: Hakuna nyongeza
2: Walimu hawapandishwi madaraja
3: Madai yao hayajalipwa kama pesa za kujikimu,uamisho etc
4: Mazingira wanayoishi ni magumu sana hasa vijijini
5: Vifaa vya kufundishia kwa vijijini hakuna.

Serikali inawasahau sana walimu na kushindwa kutatua matatizo yao ? Kutokana na malalamiko yao inaweza kuwa chanzo cha matokeo mabovu ?

Je ni kweli walimu hawana thamani ?

SOMA NA HII:  Siemens kunufaisha vyuo vikuu Tanzania kwa maendeleo ya ujuzi wa digitali

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.