Sambaza:

Kumekuwa na ukimya kuhusu suala la kuvamiwa kwa studio ya Tongwe record na kutekwa kwa baadhi ya wasanii wake akiwemo Roma, Moni Centrozone, producer wa Tongwe Records, Bin Laden na vijana wengine.

Jitihada za awali zilizofanywa na watu wao wa karibu, akiwemo mke wa Roma,Nancy zimegonga mwamba. Katika mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari, Nancy amesema amezunguka katika vituo vingi vikubwa vya polisi kuulizia taarifa za mumewe jibu analokutana nalo ni ‘hatuna taarifa zozote, tutashughulikia.’

Je ni kweli kuwa Serikali haina na haijui lolote mpaka sasa? Na kama Serikali inajua kwanini ikae kimya? Kama Serikali inawashirikilia kwa makosa yoyote kwa nini isitoe taarifa? Na kama hawapo mikononi mwa vyombo vya Serikali, wapo wapi ?

SOMA NA HII:  Ifahamu Simu ya Tecno S1 na Bei yake Nchini Tanzania

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako