Blogging

Je natakiwa kumiliki website au blog ?

on

Kila mtu ananiuliza kuhusu blogs. Ni nini? Je, ninawezaje kumiliki blog? Nitaipata wapi?

Kwa hiyo nitajibu baadhi ya maswali haya katika jarida la mwezi huu (month newsletter). Na hasa nataka kujibu swali la… “Je natakiwa kumiliki blog?”

‘Blog’ ni nini?

Kwa lugha rahisi, blogu ni gazeti la mtandaoni linalohifadhiwa kwenye tovuti. Kama ilivyo kwa diary yako, unafanya maingizo yanayoitwa machapisho (posts) kwenye blogu yako. Maingizo haya yanarekodiwa na kutumwa kwenye tovuti yako ya blogu (blogging website). Hata hivyo, tofauti na jarida la karatasi, kile unachoandika kinapatikana dunia nzima ili watu waweze kusoma.

Kwa nini unapenda mtu asome jarida lako?

Jibu ni rahisi, kwa sababu una kitu cha kushirikisha watu wengine. Blogu sio tu kuhusu mawazo yako ya kina, fikra binafsi (ingawa inaweza kuwa). Ni kuhusu chochote kinachokuvutia. Hiyo ni moja ya uzuri wa blogu – unaandika juu ya kile unachojua au kinachokuvutia. Kwa hiyo blog yako inaweza kuwa inahusu kitu chochote – mambo ya biashara, masuala ya kitaalamu, hata hobby. Kuna blog za aina nyingi mtandaoni kuna blogu ambazo ni viungo tu vya sasisho katika blogs nyingine.

Una maanisha ninaweza kuandika juu ya chochote ninachotaka?

Yep, chochote unachotaka. Ni vizuri kukumbuka kuwa blogu zilizofanikiwa zaidi – blogu zenye maana ambazo zinasomwa mara nyingi na idadi kubwa ya watu – zinahusu mada maalum. Chagua mada inayokuvutia sana, biashara au binafsi, na kisha toa taarifa zenye umuhimu.

Tuchukulie unamiliki duka la baiskeli. Una tovuti nzuri yenye kurasa za kawaida – kuhusu duka lako, kuhusu bidhaa unazoziuza, masaa ya kazi na mahali ulipo, kalenda ya matukio, nk. Una baadhi ya makala zilizoandikwa vizuri kuhusu jinsi ya kuchagua baiskeli sahihi, vifaa gani vya kuzingatia na kadhalika.

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kuondoa Visual Editor Mode Kwenye WordPress

Unapenda baiskeli na unapenda kuzizungumzia. Mtu anapokuja dukani unafurahi sana kushirikisha ujuzi wako wa miaka mingi.

Kwa ujuzi wako na shauku, unaweza kuwa na blogu nzuri sana. Fikiria kuwa na uwezo wa kushirikisha hadithi za baiskeli, kutoa habari kuhusu matukio yajayo, na kutoa maelezo juu ya baiskeli nzuri. Unaweza kuchambua vifaa na hata masoko ya bidhaa mpya na mauzo. Zaidi ya hayo, blogu yako inaweza kujibu maswali unayoulizwa kila siku na watu katika duka lako. Baada ya yote, kuna watu wengi ndani ya nchi, na kwenye mtandao ambao wana maswali sawa. Kwa hivyo blogu ni kama maisha yako – na inaongeza faida kubwa kwenye maisha ya msomaji wako. Na … blog iliyoandikwa vizuri inaweza kuongeza mauzo.

Kwa hiyo, ni nini kinachofanya blog iwe tofauti na tovuti?

Naam, blogu ni tovuti. Tofauti ni jinsi maudhui ya tovuti yanavyoongezwa, kuchapishwa, kupangiliwa na kusimamiwa.

Tovuti yako imeundwa na kurasa za kibinafsi ambazo zina muundo wako, navigation links na maudhui yako ndani yake. Kila ukurasa ni tofauti kwa sababu maudhui ni tofauti. Ili kurekebisha maudhui kwenye ukurasa unatakiwa ‘kufungua’ ukurasa huo na uhariri maudhui yake. Ili kuongeza maudhui mapya unatakiwa kutengeneza ukurasa mpya, kuandika maudhui yako na kisha uunganishe (link) kwenye kurasa zingine. Haya yote yanafanyika manually na mara nyingi inahitaji uwe na ujuzi wa kiufundi. Mara nyingi hii inasababisha tovuti kutowekwa vitu vipya mara kwa mara.

Mara nyingi blogu zinawekwa vitu vipya mara kwa mara. Zinatumia “instant publishing tools” ambazo kuongeza, kuboresha, kuhariri na kutengeneza blogu yako huwa katika mfumo rahisi – hata kwa mtumiaji mwenye uzoefu mdogo wa kompyuta. Kuchapisha mara kwa mara (Instant publishing) kunamaanisha kwamba unachotakiwa kufanya ni kuandika maudhui yako katika chombo chako cha blogu (programu) unayotumia na kisha kuichapisha. Mfumo wako wa blogu huongeza vitu moja kwa moja kwenye blogu yako, inatengeneza kurasa mpya na kusimamia mambo mengine. Maingizo yanawekwa katika utaratibu wa tarehe na, mara nyingi, hupangwa katika makundi ya mada unayounda. Kwa hivyo blogu mara nyingi, ni rahisi sana kuhariri mara kwa mara.

SOMA NA HII:  Facebook imesai deal kubwa na Universal Music

Kwa nini siwezi kuachana na tovuti ili niwe na blogu tu?

Blogu inapangiliwa kwa tarehe ya kuingia, kama kurasa za jarida lako. Tovuti, hata hivyo, imeandaliwa kwa njia zinazoongoza kuelekea malengo maalum. Kwa mfano, ikiwa unauza huduma fulani, utakuwa na kurasa chache za maudhui kuchukua wageni wako kupitia mtiririko wa mauzo. Haiwezekani katika blogu.

Kutumia blogu pekee, mchakato huo wa mauzo utafichwa ndani zaidi kwenye tovuti unapoongeza maudhui zaidi. Kwa hiyo wakati blogu inafanya kazi kama gazeti, sio bora – peke yake – kwa biashara kwa sababu ya jinsi ya kupanga maudhui yako.

Sasa ni kitu gani kingine cha pekee kuhusu jambo hili la blogu?

Kuna Vipengele vingine viwili muhimu … Maoni na Injini za Utafutaji (Comments & Search Engines).

Maoni

Mara nyingi bloggers (watu wanaomiliki blog) huwawezesha watumiaji wa blog zao kutoa maoni kwenye mada za blogu zao. Hii inawapa watumiaji hisia ya uhusiano, jamii na kuona kwamba wana thamani. Kwa kuongeza, hujenga kiwango cha juu cha maslahi kwa watumiaji ambao mara nyingi watataka kuingia kwenye blog yako ili kuona vitu vipya au kutoa maoni zaidi. Wakati watu hao hao wanatembelea mara kwa mara na kutoa maoni kwenye blogu yako, hii inaweza kusababisha kujenga jumuiya ya asili inayoendelea – yote kuhusu mada yako – na yote yanayotokana na vitu unavyoandika. Unaweza kuelewa jinsi aina hii ya jumuiya inavyoweza kukusaidia katika biashara yako.

SOMA NA HII:  Akismet ni Nini na Kwa Nini Unatakiwa Kuitumia Kwenye Tovuti Yako

Injini za Utafutaji (Search Engines)

Injini za utafutaji zinaonekana tu zinapenda blogu. Hasa Google. Mbali na hilo, blogu huwa na mwelekeo wa mada – ambao injini za utafutaji zinapenda. Pia huwa na mabadiliko mara kwa mara – injini za utafutaji zinapenda maudhui mapya. Na blogu huwa zinajenga trafiki kwa kasi zaidi kuliko tovuti ambazo sio blogu kutokana na ushiriki wao kwa jamii – trafiki zaidi, ndio kuwa kwenye nafasi ya juu kwenye injini ya utafutaji. Kumbuka kwamba kama vile ilivyo kwa tovuti yako, na blogu si njia fupi ya kuwa namba # 1 kwenye Google. Bado inahitaji mipango, juhudi, muda, kuendelea na uvumilivu wa kujenga cheo kwenye injini ya utafutaji (search engine rankings). Na blog inaweza kusaidia na hilo.

Mwisho …

Natumaini, nimekupa maelezo ya kina kuhusu blog na jinsi gani inaweza kusaidia biashara yako. Mpaka hapa, unapaswa kuwa na uwezo wa kujibu swali, “Je, natakiwa kuwa na Blog?” Ikiwa huna, au una maswali au unataka kujadili kama blogu inafaa katika mahitaji yako ya biashara, tafadhali wasiliana na mimi kwa njia yoyote hapa kwenye mediahuru na tuweze kuweka ratiba ya muda mzuri wa kuzungumza.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.