Maujanja

Je kuna madhara ya kuacha simu/laptop kwenye charge kwa muda mrefu

Mara kwa mara nimekuwa nikikutana na swali hili kutoka kwa wadau wakitaka kujua kama kuna madhara ya kuacha simu au laptop kwenye charge kwa mda mrefu hata kama imeishajaa chaji ?

Wengine wanataka kujua ikiwa wataacha simu zao za mkononi kwenye charge usiku mzima kuna kuwa na madhara gani na nini kinatokea ikiwa simu imeshajaa kikamilifu lakini bado imeunganishwa kwenye umeme ?

Kwa uzoefu wangu haina madhara kwa sababu mara baada ya betri kujaa kikamilifu (fully charged) haitapokea nishati yoyote kutoka kwenye charger, kwa sababu viwango vyote vya nishati ambayo ilikuwa inahitajika betri ilipo kuwa tupu sasa vinakuwepo.. Kwa mfano katika betri ya Lithium ion  wakati “ions” zote zimefika kwenye “electrode” sahihi upinzani dhidi ya nishati zaidi unakuwa mkubwa sana.

Lithium batteries ndio teknolojia ya betri inayotumika kwa sana hivi sasa. Haziathiriwi sana kutokana na kuwa na uwezo wa kusimamia kinachoingia na kinachotoka kwenye betri pia zinazuia “overcharging” na “overdraining”.

Kitaalamu hakuna madhara ya kuacha simu au laptop kwenye charge kwa muda mrefu ila ni bora kuchomoa chaja wakati haitumiwi.

Please subscribe to our newsletter

SOMA NA HII:  Tumia .tz domain upate faida kuu 5 kwenye biashara yako
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

1 maoni kwenye “Je kuna madhara ya kuacha simu/laptop kwenye charge kwa muda mrefu”

JIUNGE NA MAZUNGUMZO, TOA MAONI YAKO HAPA

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Lako