Nyingine

Jay Moe alivyopata aibu baada ya kumdharau Billnass

Msanii anayenafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Nisaidie Kushare’ , Jay Moe amesema licha ya kutamani kufanyakazi na rapa wa wimbo ‘Sitaki Mazoea’, Billnass lakini hatasahau alivyomdharau kabla ya kusikiliza na kuona video zake.

Rapa huyo amedai hakuwa akijua uwezo mkubwa alionao rapa huyo hivyo hata alipotumiwa wimbo wa rapa huyo na meneja wake alidharau hakuusikiliza hadi walipokutana nchini Afrika Kusini.

Kupitia gazeti la Mtanzania, Jay Moe amesema:

“Unajua kuna siku meneja wake, Bill Nas ‘Mchafu’, alinitumia wimbo akiniomba niwatumie na wengine lakini mimi sikufanya hivyo, nilipowakuta Afrika Kusini na kuwahoji wakaniambia wapo kwa ajili ya kufanya video ya wimbo alionitumia, nilijisikia vibaya sana na niliona aibu maana niliona video yake ni kali tofauti na nilivyokuwa nikimdhania,”

“Hapo nikajifunza kitu kuwa hutakiwi kumdharau mtu, maana dogo ana uwezo mkubwa wa kurap na anajua nini anafanya hadi nimemwahidi kufanya naye kazi,” alisema Jay Moe.

SOMA NA HII:  Idara ya Habari (MAELEZO) Yapokea Msaada wa Vifaa Kutoka Ubalozi wa China

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako