Ipi ni sahihi, Tanzania “Lipa kwa M-Pesa” au Kenya “Lipa na M-Pesa” ?


Ujumbe rahisi wa kuhamisha fedha kwa njia ya simu umefungua mjadala juu ya tofauti kati ya Kiswahili kinachozungumzwa nchini Kenya na Tanzania.

Kwa hiyo, swali ni: Je Safaricom wanakosea wanaposema Lipa na M-Pesa? Naam, Watanzania wanafikiri hivyo. Tanzania unaambiwa Lipa kwa M-Pesa.

Ishara inayowaambia wateja nchini Tanzania kuwa lipa kwa na Kenya lipa na imezua mjadala kwa watu wengi na wanauliza ni nani yupo sahihi kati ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa mhariri wa Taifa Leo Juma Namlola, Wakenya hawapendi kutumia maneno na misamiati sahihi hasa wakati wanaongea Kiswahili.

“Neno, na na kwa, hutumiwa tofauti na pia kwa matukio tofauti. Grammatically kwa ni neno sahihi la kutumia, “alisema Namlola.

Lakini Wakenya wote wanakubaliana? Na kwa mtazamo wako, ni kampuni gani imetumia neno sahihi?

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA