iPhone X vs Samsung Galaxy Note 8 – Simu gani ni nzuri kununua ?


Ikiwa una pesa nyingi ya kutumia kwenye kununua simu mpya lakini haujui uingie kwenye familia gani kati ya (Android au Apple) mawazo yangu ni kuwa, uamuzi wako utaangukia kwenye moja ya vifaa viwili vikubwa kwa sasa: iPhone X au Galaxy Note 8.

Wakati Apple inaitangaza simu yake ya hivi karibuni kama “future of smartphones” shukrani kwa uwezo wake wa kutambua uso na kioo chenye mvuto, wengine wanaweza kusema kwamba Samsung ndiyo bora zaidi, na Galaxy Note 8 inajivunia sifa kama hizi kwa sababu ilitoka miezi kadhaa iliyopita .

Tumelinganisha uwezo wa iPhone X na Galaxy Note 8  ili kuona ni ipi inastahiki fedha zako.

USANIFU

 • iPhone X:- 143.6×70.9×7.7mm, 179g
 • Galaxy Note 8:- 162.5×74.8×8.6 mm, 195 g

Jambo la kwanza: usanifu. IPhone X sio tofauti sana na Galaxy S8 linapokuja swala la muonekana. Simu zote mbili zina kioo kilichofunika sehemu yote ya mbele na kimezungukwa na fremu ya chuma, na zote mbili zina “bezel-less displays”. Tofauti na Galaxy S8, ambayo ina kioo kilichofunika sehemu yote ya mbele , iPhone X ina sehemu ndogo iliyoachwa sehemu ya juu ya kioo, ambapo kuna kamera ya mbele na sensors.

IPhone X ni nyepesi zaidi kuliko Note 8, ina 179g ikilinganishwa na 195g, na pia ina umbo zuri zaidi hivyo inatosha kukaa vizuri kwenye mfuko wako wa jeans, ni nyembamba zaidi ya 4mm kuliko simu ya Samsung.

Hata hivyo, hii ni kwa sababu ya ukubwa wa kioo cha Note 8, kwa hiyo inategemea ni kitu gani unapenda zaidi. Kioo kikubwa au kidogo, lakini simu zote mbili ni sawa sawa linapokuja swala la kukaa vizuri kweye mfuko wa jeans.

SOMA NA HII:  Njia 5 za Kufanya Kuchat Kuwe na Mvuto Zaidi

IPhone X pia ni ndogo kidogo, ina unene wa 7.7mm ikilinganishwa na unene wa 8.6mm wa Note 8.

Kwa upande wa rangi , iPhone X itakuwa inapatikana katika rangi ya Space Grey na Fedha, wakati Galaxy S8 inapatikana katika Midnight Black, Gray Orchid, Arctic Silver, Coral Blue na Maple Gold.

KIOO

 •  iPhone 8:- 5.8in Super Retina (2436×1125, 458ppi) OLED edge-to-edge display
 • Galaxy Note 8:- 6.3in Super AMOLED (1440×2960, 521ppi) edge-to-edge

Galaxy Note 8, yenye  kioo chenye inchi 6.3 Super AMOLED, mara nyingi inashinda vita yoyote dhidi ya iPhone kwa matoleo yake yaliyopita. Hata hivyo, sasa ina mshindani mzuri kwa ujuo wa iPhone X, ambayo ni ya kwanza kwa smartphone za Apple kuwa na edge-to-edge display.

Ingawa haijajikunja kama ile ya kwenye Note 8, iPhone X’s 5.8inch OLED imeinuliwa kidogo ili kujaza sehemu ya mbele ya simu. Zaidi ya hayo, kioo muonekano cha ‘Super Retina’ kwenye iPhone X, kikiwa ni 2436 × 1125 na 458ppi, ni skrini kubwa zaidi kuwekwa kwenye simu za iPhone, na ya kwanza kutumia OLED na Apple True Tone tech, ambayo hubadilisha mwanga wa skrini kuendana na mazingira yako.

 VIFAA NA UHIFADHI (STORAGE)

 • iPhone X:- A11 Bionic CPU, 3GB RAM, 64GB au 256GB storage
 • Galaxy Note 8:- Exynos 8995 octa0core CPU, 6GB RAM, 64GB storage, microSD hadi 256GB

IPhone X imetambulisha prosesa mpya ya Apple inayoitwa A11 Bionic CPU. Prosesa hii ina kasi zaidi kuliko ya awali.

Galaxy Note 8, inakuja na prosesa ya Samsung inayoitwa octa-core Exynos 8995, ambayo ina cores mbili zaidi kuliko prosesa mpya ya Apple.

SOMA NA HII:  Ifahamu Simu ya Huawei Nova 2S Bei na Sifa Zake

Kwa upande wa memori , iPhone X ina RAM ya 3GB, ikilinganishwa na mara mbili ya hiyo katika Note 8, ambayo ina 6GB, na uhifadhi wa ndani (storage) wa 64GB au 256GB . Ingawa Galaxy Note 8 inapatikana katika uhifadhi wa ndani wa 64GB tu, inawapa watumiaji uwezo wa kupanua kwa kuweka memori, kitu ambacho iPhone X haina.

PROGRAMU

 • iPhone X:- iOS 11
 • Galaxy Note 8:- Android 7.0 Nougat

Huwezi kamwe kulinganisha Android na iOS, kwa sababu kwa sababu karibu kila mtu ana mapendekezo yake mwenyewe linapokuja swala la mfumo wa uendeshaji ambao anatumia.

IPhone X inatumia iOS 11, inakuja na vipengele vipya na vizuri zaidi, ikiwa ni pamoja na  ‘Animoji’, ishara mpya za kutumia simu, multitasking, portrait lighting na selfie modes.

Galaxy Note 8 inatumia Android Nougat inawezesha kifaa hiki huku ikiwa na vipengele vipya, ikiwa ni pamoja na Apps Galaxy na Samsung Gallery app.

Simu zote zina teknolojia ya “face-scanning”, huku iPhone X ikianzisha ‘Face ID’, ambayo Apple inadai ni teknolojia sahihi zaidi na salama ya uthibitisho wa sura.

Teknolojia ya “face-scanning” kwenye Note 8 sio nzuri sana, lakini Samsung inawawezesha watumiaji kutumia “fingerprint scanner”, wakati Apple imeweka pamoja Touch ID.

KAMERA

 • iPhone X:- Dual 12MP (f/1.8 na f/2.4) na OIS, 7MP front-facing
 • Galaxy Note 8:- Dual 12MP (f/1.7 na f/2.4), 8MP front-face

IPhone X ina kamera mbili sawa na kwenye iPhone 7 Plus. Hata hivyo, kihisio (sensors) mbili za 12MP zimeboreshwa.

Galaxy Note 8 nayo ina mipangilio sawa, ikiwa na kamera mbili zenye 2x optical zoom na uwezo wa kurekodi picha wa 9MP.

SOMA NA HII:  Fun Time! Taja Simu Yako Ya kwanza Kutumia Na Ulinunua Ama Ulinunuliwa?

BETRI

 • iPhone X:- inakaa masaa 21, uwezo wa kuchaji kwa haraka, kuchaji bila waya (wireless charging)
 • Galaxy Note 8:- 3,300mAh, uwezo wa kuchaji kwa haraka, kuchaji bila waya (wireless charging), USB-C

Apple haijafanya mabadiliko makubwa kwenye ukubwa wa betri ndani ya iPhone X, lakini wamesema kwamba ina uwezo wa kukaa masaa mawili zaidi kuliko iPhone 7 na kukupa saa 21 za majadiliano.

Galaxy Note 8 ina betri yenye ujazo wa 3,300mAh, ambayo kwa ukubwa wake, inaweza kuonekana nzuri . Hata hivyo, Kwa Simu ya ukubwa huu, betri 3,330mAh inaonekana kuwa ndogo, hasa ikilinganishwa na betri ya 3,500mAh kwenye Galaxy S8.

BEI

 • iPhone X:- Kuanzia £999
 • Galaxy Note 8:- Kuanzia £869

Ingawa ina orodha ya sifa nzuri zaidi kwa simu za iPhone, Simu mpya ya Apple pia inatarajiwa kuwa ya gharama kubwa zaidi kwa simu za Apple hadi sasa, bei inaanzia  £ 999 kwa toleo lenye 64GB.

Hata hivyo, Galaxy Note 8 haipo mbali, inapatikana kwa bei kuanzia £ 869, na kufanya iPhone X kuwa na bei ghali zaidi kwa kiasi cha  £ 130  kuliko simu ya Samsung.

MAJIBU YETU

IPhone X na Galaxy Note 8 ni sawa kabisa kwa suala la kile wanachotoa, kwa mfano: miundo ya kioo, kioo chenye mwanga mzuri na kufanya kazi kwa haraka kutokana na kuwa na prosesa zenye uwezo mzuri.

Hata hivyo, bado kuna tofauti muhimu. Wakati iPhone X inaizidi Galaxy Note 8 kwa ubunifu zaidi , Note 8 ina kioo bora zaidi, uwezo mzuri wa  ndani na sehemu ya memori (microSD).

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA