iPhone mpya itakuwa na “infrared face unlock” – Ripoti

Apple kwa bahati mbaya wametoa firmware kwajili ya HomePod, ambayo ina maelezo kuhusu simu mpya iPhone kutoka kwa kampuni hiyo, The Verge imeripoti.

Firmware ilibainisha kwamba iPhone ijayo itakuwa na “infrared face unlock” katika BiometricKit, na msanidi programu (developer) Steve Troughton-Smith kupitia mtandao wa twitter ameweka screenshots kuhusu firmware hiyo.

Pia aliweka picha kutoka kwenye firmware ambayo inaonekana kufafanua kipengele cha chini cha muundo wa iPhone ijayo.

Apple inatarajia kuzindua iPhone mpya hivi karibuni – tetesi zinasema itakuwa iPhone 8 – itatoka baadaye mwaka huu.

Vipengele vingine vinavyotarajiwa kuwemo kwenye simu hiyo ni pamoja na muundo wa kioo-kwa nyuma na wireless charging.

SOMA NA HII:  HTC yazindua simu mbili mpya HTC U11+ na U11 Life

COMMENTS

WORDPRESS: 1
  • comment-avatar
    Baraka 6 months

    sidhani kama ni sehemu sahihi kuandika ujumbe huu ila nimeipenda tovuti yenu maana mnaandika habari za tehama kama habari zingine tofauti na tovuti nyingine ambazo huelezea vitu ambavyo msomaji unashindwa hata kuelewa