Sambaza:

Infinix S2 Pro (a.k.a Infinix X522) na simu ya Infinix S2 ni wafuasi wa Infinix Hot S. Infinix inaonekana kuachana na branding ya Hot kwenye simu za Infinix S kama walivyofanya kwenye aina ya simu za NOTE miaka michache iliyopita. Kipengele bora zaid kwenye Infinix S2 Pro ni kamera mbili za mbele, ambazo zinawavutia zaidi wapenzi wa selfie na wefie.

Sifa Muhimu za Infinix S2 Pro

  • 5.2-inch IPS Display, 720 x 1280 pixels (282 ppi)
  • 1.3GHz octa-core MediaTek MT6753 CPU with 2GB / 3GB RAM
  • Android 6.0 (Marshmallow)
  • 16GB or 32GB Storage with support for memory card up to 128GB
  • 13MP Rear Camera and 13MP + 8MP Front Camera
  • 4G LTE (up to 150 Mbps download)
  • Fingerprint Sensor
  • 3000 mAh Li-ion Battery with Fast Charging
SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno Phantom 6 Plus bei na Sifa zake

Infinix S2 Pro

Muonekano na Kioo

Infinix S2 Pro ni simu janja mpya yenye mwonekano mzuri sana. Simu hiyo imekuja na ukubwa wa kioo cha nchi 5.2 chenye teknolojia ya IPS LCD (720 x 1280 pixels).

Kwa upande wa wapenzi wa Kamera Infinix S2 Pro haijambo pia. Kuwa na kamera mbili upande wa mbele ni kitu kinachozungumziwa sana. Infinix S2 Pro ina kamera mbili za mbele moja ya 13 megapixels na nyingine ya  8 megapixels.

Kamera ya nyuma kwenye Infinix S2 Pro ina 13 megapixels na mfumo wa dual-LED flash ili kukuwezesha kupiga picha nzuri hata kwenye maeneo yenye mwanga mdogo.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno W5 bei na Sifa zake

Vifaa na Programu

Kwa upande wa mfumo endeshi, simu ya Infinix S2 Pro inaendeshwa na toleo la Android 6.0 (Marshmallow), pamoja na Betri yenye ujazo mkubwa wa 3000mAh.

Prosesa yake ni ya 1.3GHz MediaTek MT6753 chipset. Kwa upande wa ndani yaani diski uhifadhi (internal storage) ukubwa wake ni 32GB pamoja na RAM ya 3GB. Ingawa toleo la kawaida la Infinix S2 lina diski uhifadhi ya ukubwa wa 16GB na 2GB RAM.Pia unaweza kuweka memori ya nje yenye ukubwa mpaka 128GB.

Vitu vingine utakavyopata kwenye Infinix S2 Pro ni Fingerprint, Wi-Fi, GPS, Bluetooth, FM Radio, na inasapoti mfumo wa 3G na 4G.

SOMA NA HII:  Tecno Camon C8 vs Tecno Boom J8 – Ninunue simu gani ?

Bei na Upatikanaji

Infinix S2 Pro inapatikana Tanzania, Nigeria, Kenya, na Ghana. Unaweza kununua simu janja hii ya Adroid kwenye maduka ya mtandaonikwenye nchi husika. Bei ya Infinix S2 Pro kwa Tanzania ni kati ya Tsh 360,000 hadi Tsh 460,000, inategemea na eneo ulilopo.

Infinix ni watengenezaji wa simu walio na makao makuu yao huko nchini Uchina katika mji wa Pudong. Ilianza kutoa huduma tangu mwaka 2012 na maeneo makubwa ya biashara zake ni bara la Afrika na Asia. Pia, Infinix inadai kuwa matawi katika nchi zaidi 60 duniani kote.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako