Imevuja: Sony Xperia XZ2 Premium kuja na Android 9.0 P, Kamera mbili na SD 845 chipset


Uwepo wa Sony katika mkutano wa MWC 2018 uliofanyika mwezi Februari ulifanya tuone uzinduzi wa simu ya Sony Xperia XZ2. Hata hivyo, Kampuni hiyo kutoka nchini Japani inazidi kuwavutia wapenzi wa simu hiyo kwa kutengeneza simu bora zaidi, sasa wana mpango wa kuja na simu ya Sony Xperia XZ2 Premium. Simu hii inatarajiwa kuingia sokoni mwishoni mwa mwaka 2018 (labda tutaona uzinduzi wake katika IFA 2018) lakini leo, sisi tayari tunafahamu vitu vinavyotarajiwa kuwepo kwenye simu hii.

Sony Xperia XZ2 Premium
Kwa mujibu wa taarifa zilizovuja, Xperia XZ2 Premium itakuwa na skrini ya 6.01-inch ambayo itabeba resolution ya 4360 x 2160 pixels. Chini ya skrini hii ya LCD kutakuwa na mfumo wa uendeshaji wa Android P ambao unatarajiwa utakuwa tayari umezinduliwa wakati huo.

Zaidi ya hayo, toleo la Premium la XZ2 litakuwa na Qualcomm Snapdragon 845 chipset ambayo kitakuwa na ndoa na 6GB ya RAM. Pia, inatarajiwa kuwa na fingerprint kwa nyuma.

Simu hii haitarajiwi kuwa na na bei nafuu,ukizingatia kuwa itakuwa flagship ya mwaka. Hiyo ni pamoja na uzoefu kwamba simu za mkononi za Sony zinauzwa bei kubwa. Kwa sasa, hakuna tunachokijua zaidi ya hapo. Mara tu maelezo zaidi yatakapotokea, tutakuwa wa kwanza kukujulisha.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *