Ifahamu simu ya ZTE Tempo Go bei na Sifa zake


Wakati wa MWC 2018, ZTE Tempo Go ilikuwa moja ya simu za bei nafuu zilizo zinduliwa na kuunga mkono toleo la Android Go OS. Mkakati huu unahusisha simu janja zenye uwezo mdogo kama RAM 1G na chini ya hapo kama vile ZTE Tempo Go. Tofauti na OS ya kawaida, Toleo la Go limefanyiwa marekebisho na lina uzito mzuri ili uweze kutumia vizuri na kuchukua nafasi ndogo kwenye simu janja yako.

Sifa muhimu za ZTE Tempo Go

  • 5.0-inch, TFT capacitive touchscreen, 854 X 480 pixels, 854 X 480 pixels (196 ppi)
  • Quad-core Qualcomm MSM8909 Snapdragon 210 with 1GB RAM
  • 8GB built-in storage, up to 32GB with a memory card
  • 5MP rear camera and 2MP front camera
  • 4G LTE
  • 2, 200mAh removable Li-ion battery

Muonekano na Kioo

ZTE Tempo Go ina muonekano mzuri kidogo kuliko baadhi ya ndugu zake katika entry level. Kila kitu kiwekwa vizuri. ZTE Tempo Go ina kioo chenye ukubwa wa 5.0-inch na resolution ya 854 X 480 pixels kama ilivyo kwa Nokia 1.

Betri na Kamera

Ina uwezo wa kutosha wa betri ambao sio mkubwq lakini unatosha kutumikia hadi siku nzima kwa matumizi ya kawaida. Betri yake ina ukubwa wa 2, 200mWh Li-ion.

Kwa wapenzi wa picha, ZTE Tempo Go inakuja na kamera ya nyuma ya 5MP na kamera ya mbele ya 2MP. Mpangilio huu kwa sasa ndio unaotumika kwenye simu janja nyingi za bei nafuu (entry level smartphones).

Vifaa na Programu

Ingawa, simu janja hii inatumia Qualcomm chipset bado bado ina uwezo mdogo ikiwa na kasi ya 1.1GHz tu. Simu hii inakuja na  Quad-core Qualcomm Snapdragon 210 na Adreno 304 GPU kwa ajili ya graphics.

Simu hii pia ina RAM ya  1GB pamoja na hifadhi ya ndani ya 8GB inayoweza kuongezwa kwa kuweka memori kadi hadi ya 32GB.

Bei na Upatikanaji

Simu hii ya mkononi inapatikana kwenye tovuti ya kampuni kwa karibu $80 ambayo ni takriban 180, 000 katika Tsh.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA