Tecno WX3 na Tecno WX4 ni simu za android za kiwango cha kati zikiwa na vipengele vingi vinavyovutia , zote zinatumia mfumo endeshi wa Android 7.o Nougat na HiOS.

Simu za “WX” ni matawi ya mfululizo wa Tecno “W” smartphones za bei nafuu, ni kama Tecno W3, W4 na W5. Mfululizo wa WX umeboresha mfumo wa uendeshaji huku zikiwa na bei nafuu sana.

Tecno WX4 ina screen resolution kali na fingerprint scanner nyuma ya simu, pia ina uwezo mkubwa wa betri, kuhusu betri, WX3 ina Pro version iliyo na betri yenye 5000 mAh.

Sifa na Uwezo wa Tecno WX4

Tecno WX4

Simu ya WX4 ina ukubwa sawa wa skrini kama simu ya tecno WX3 lakini ina screen resolution bora zaidi. Skrini ina ukubwa wa inchi 5.0  na resolution ya pixels 1280* 720 .

Inatumia HiOS kulingana na Android 7.0 Nougat ambayo imekuwa pointi muhimu kwenye mauzo ya simu hii, hifadhi ya ndani ya 16GB inatosha sana. WX4 ina fingerprint scanner ambayo imewekwa nyuma kwa usalama wa kutosha na kufungua simu yako kwa rahisi.

SOMA NA HII:  Simu 10+ bora za Tecno na Bei zake nchini Tanzania

Simu hii inawezeshwa na processor ya quad-core 1.3GHz na Mediatek chipset,ikiwa na  RAM ya 1GB inaweza kutosha kukupa matumizi salama wakati wa multitasking.

Tecno WX4 ina kamera ya nyuma ya megapixel 8 na LED flash moja , kamera ya mbele pia ina megapixel 8 na LED flash ili kuongeza ubora wa picha katika hali yenye mwanga hafifu.

Ina betri yenye uwezo wa 2800 mAh, WX4 ni simu la laini mbili na inapatikana katika rangi ya Rose Gold, Champagne Gold, Anthracite Grey na Elegant Blue. Kifaa hiki hakina huduma ya 4G.

Sifa Zingine za Tecno WX4

 • Mfumo wa Uendeshaji: Android 7.0 Nougat With HiOS
 • Ukubwa wa Kioo: 5.0 inches FWVGA screen. 720 x 1280 pixels (297 PPI)
 • Chipset: MediaTek
 • Uwezo wa Processor: Quad-core 1.3 GHz
 • Uwezo wa RAM: 1GB RAM with  ROM with SD card support (32GB)
 • Ukubwa wa Ndani: 16GB
 • Ukubwa wa Nje: microSD, mpaka ukubwa wa 32GB
 • Kamera ya Nyuma : 8 MP na LED flash
 • Kamera ya Mbele: 8 MP na LED flash
 • Uwezo wa Mtandao: 3G
 • Uwezo wa Battery: 2800 mAh Battery
 • Accelerometer, gyro, proximity and fingerprint sensor.
 • FM Radio: Ndio
 • Bluetooth: v4.0
 • WiFi: Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, hotspot
 • GPS: Ndio
SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Infinix Zero 5 Pro bei na Sifa zake

Sifa na Uwezo wa Tecno WX3

WX3 ilikuja kwa matoleo matatu tofauti, toleo la msingi ambalo ni Tecno WX3, haina uhusiano wa mtandao wa 4G na ina betri ya 2500 mAh.

Toleo la pili ni Tecno WX3 LTE ambalo ina lina mtandao wa 4G na betri sawa ya 2500 mAh, Tecno WX3 Pro ni toleo la mwisho.

WX3 Pro ina betri yauwezo wa 5000 mAh, mara mbili ya toleo la kwanza  lakini haina chaguo la Mtandao wa 4G.

Sifa Zingine za Tecno WX3

 • Mfumo wa Uendeshaji: Android 7.0 Nougat With HiOS
 • Ukubwa wa Kioo: 5.0 inches FWVGA screen. 720 x 1280 pixels (297 PPI)
 • Chipset: MediaTek
 • Uwezo wa Processor: Quad-core 1.3 GHz
 • Uwezo wa RAM: 1GB RAM with  ROM with SD card support (32GB)
 • Ukubwa wa Ndani: 8GB
 • Ukubwa wa Nje: microSD, mpaka ukubwa wa 32GB
 • Kamera ya Nyuma : 5 MP na LED flash
 • Kamera ya Mbele: 5 MP na LED flash
 • Uwezo wa Mtandao: 3G (3G na 4G kwenye WX3 LTE)
 • Uwezo wa Battery: 2500 mAh Battery
 • Accelerometer, gyro na proximity
 • FM Radio: Ndio
 • Bluetooth: v4.0
 • WiFi: Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, hotspot
 • GPS: Ndio
SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno Spark Plus K9 bei na Sifa zake

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako