Ifahamu simu ya Tecno Spark Plus K9 bei na Sifa zake


Tecno Spark Plus K9 ni simu mpya na ya kisasa zaidi kutoka Tecno Mobile kwa hakika inastahili kuwa mgombea mzuri katika jamii ya simu za Android zenye bei ndogo.

Tecno Spark Plus K9 haikuja peke yake, iliongozana na Tecno Spark K7 ambayo ina bei ndogo na vipengele vya chini ikilinganishwa na Spark Plus K9, simu mpya kwenye jamii ya simu za ‘Spark’  kutoka kwa Tecno. Angalia sifa za simu za Tecno Spark hapa chini.

Tecno Spark Plus K9Simu zote mbili Tecno Spark Plus K9 na Spark K7 ni simu za bei nafuu ambazo zina vipengele vya kuvutia na muundo mzuri, ingawa dhana ya kuzibuni inaweza kuwa imetolewa kwenye simu ya iPhone 7.

SOMA NA HII:  Uchambuzi wa simu ya Infinix Hot S X521 na Bei yake nchini Tanzania

Sifa kamili za Tecno Spark Plus K9 ni kama ifuatavyo:

Sifa zaidi za Tecno Spark Plus K9


Tecno K9 inatumia kioo chenye ukubwa wa inchi 6.0, ina uwezo wa 720*1280 kitu ambacho hakijanivutia sana kutokana na ukubwa wa kioo wa smartphone hii.

SOMA NA HII:  Jinsi ya kuficha (hide) picha kwenye simu za android

Ina uwezo wa uhifadhi wa ndani wa GB 16 na RAM 2 GB  ili kukupa uhuru zaidi kwenye kutumia simu hii. RAM inasaidiwa na Mediatek chipset na prosesa ya 1.5 GHz Octa-core. Kumbuka: Tecno K7 ina RAM 1GB na processor ya 1.3 GHz.

Hifadhi ya ndani ya simu inaweza kupanuliwa kwa kuweka memori kadi hadi kufikia GB 32. Tecno Spark K9 inakuja na mfumo wa Tecno HiOS 2.0 ambao umeboreshwa kulingana na Android 7.0 Nougat.

Tecno Spark Plus K9 ina kamera ya msingi ya megapixel 13 ikiwa na LED flash, kamera ya mbele ni megapixel 5 kwa madhumuni ya selfies na video call. Kamera ya mbele pia ina LED flash ili kuongeza ubora wa picha kwenye mazingira yenye giza

SOMA NA HII:  Nunua Simu za Tecno Mtandaoni kupitia ZoomTanzania & Jumia Online Stores

Simu hii ina betri yenye uwezo wa 3,400 mAh, ingawa sio bora kuliko betri zingine, uwezo wa betri kwenye Tecno Spark Plus K9 ni wa kutosha na utakupa uwezo wa kutumia simu kwa muda mrefu.

Spark Plus K9 ni simu ya laini mbili ila haitumii mtandao wa 4G, pia ina fingerprint scanner kwa nyuma kwajili ya usalama wa kufungua simu.

Bei ya Tecno Spark Plus K9 nchini Tanzania ni 260000 inaweza kupungua ama kuongezeka kutokana na eneo ulilopo.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA