Ifahamu simu ya Tecno Spark K7 bei na Sifa zake


Tecno kwa sasa inafanya kazi kuendeleza mfululizo mpya wa smartphone unaoitwa Spark series. Simu janja ya kwanza chini ya mfululizo huu itakuwa Tecno Spark K7 na kampuni hiyo imekuwa ikiitangaza kupitia mitandao ya kijamii.

Tecno Spark-mediahuru

Tecno Spark K7 itakuwa simu ya bei nafuu kutoka kwa kampuni hiyo, natarajia kuiona katika maduka ya rejareja hivi karibuni. Kukusaidia kuamua ikiwa hii ni smartphone yenye thamani ya kusubiri au la, hapa chini tunaangalia na kuchambua sifa za Tecno Spark K7 na bei yake nchini Tanzania.

Sifa kamili za Tecno Spark K7 ni kama ifuatavyo:

Kama unavyoona kwenye sifa zake hapo juu, Tecno Spark K7 kwa bei yake sio kifaa kibaya . Nadhani hizi ni sifa nzuri kwa simu ya bei chini ya Tsh 200,000. Ingeweza kuwa bora zaidi lakini nadhani Tecno hajatuangusha. Simu hii inalenga hasa wale ambao wananunua simu janja mara ya kwanza au hata wale wanataka smartphone ya pili lakini hawataki kutumia pesa nyingi katika manunuzi.

Tecno Spark K7 inakuja katika soko mwezi mmoja baada ya Infinix, inayomilikiwa na kampuni inayomiliki Tecno, ilizindua simu yake ya bei nafuu ya smartphone, Infinix Smart. Inaonekana kama mwenendo wa sasa ni kuhamia kwenye vifaa vya gharama nafuu vinavyolenga watumiaji ambao wanaweza kujisikia wameachwa njiani kutokana na gharama kubwa za simu zingine. Sehemu hii ya soko imejazwa na wazalishaji wa China wasiojulikana wengi ambao hawana uwepo rasmi katika nchi.

Zote ni vifaa vya kwanza kutoka kwa kampuni hiyo, ikiwa zitafanya kazi vizuri, tunaweza kuishia kuona muendelezo wa simu hizi katika kipindi cha miezi 12 ijayo. Mimi binafsi nadhani zitafanya vizuri kama Tecno wakizitangaza vizuri sokoni . Tecno tayari brand yake inatambulika hii itasaidia kwa mfululizo wa simu za Spark kufanya vizuri.

Endelea kutembelea hapa, nitakuwekea updated juu ya lini  simu hii itaanza kupatikana itakapo zinduliwa nchini Tanzania.

3 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA