Kampuni ya Simu za mkononi ya Tecno Mobile, leo Aprili 5, 2017 imezindua rasmi toleo jipya la simu za Tecno Camon, simu hizo mpya ni Tecno Camon CX pamoja na Camon CX Air,  uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Kilimanjaro Hoteli uliopo Posta jijini Dar es Salaam.

Tecno Camon CX

Simu hizi mpya za Tecno Camon CX pamoja na Tecno Camon CX Air zimetengenezwa maususi kwa watu wanaopenda picha “selfies”. Tecno Camon CX inakuja na Processor ya Media Tek MT6750T yenye uwezo wa 1.5GHz ikiwa pamoja na RAM ya GB 2 pamoja na Ukubwa wa ndani wa GB 16, simu hii vilevile inakuja na toleo jipya la Android Nougat au Android 7 huku ikiwa inaendeshwa na Battery yenye uwezo wa 3200 mAh ikiwa imewezeshwa kwa teknolojia ya Li-Po (Lithium polymer battery) ambayo ina uwezo wa kudumu na chaji kuanzia masaa 22 na kuendelea.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno Camon CX Air bei na Sifa zake

Kwa upande wa kioo simu hii ina kioo cha size ya inch 5.5 ikiwa na teknolojia ya IPS display chenye resolution ya 1080 X 1920 pixel, simu hizi pia zime tengenezwa na uwezo wa 3G pamoja na 4G zote zikiwa zinauwezo huo. Tukiangalia upande wa kamera Tecno Camon CX inakuja na kamera ya Mbele na nyuma zote zenye uwezo wa 16 Megapixel huku kwa mbele kamera yake ikiwa na teknolojia ya dual-LED flash pamoja na uwezo wa Auto Focus kwa kamera zote mbili ya mbela na nyuma.

Kwa kifupi hizi ndio sifa za simu mpya za Tecno Camon CX pamoja na Tecno Camon CX Air

  • 5.5-inch IPS Display, 1080 x 1920 pixels (400ppi)
  • 1.5GHz octa-core Mediatek CPU with 2GB RAM
  • Android 7.0 (Nougat) with HiOS
  • 16GB Storage with support for memory card up to 128GB
  • 16MP Rear Camera and 16MP Front Camera
  • 4G LTE (up to 150Mbps)
  • Fingerprint Sensor (Rear)
  • 3200 mAh Battery with Fast Charging
SOMA NA HII:  Uchambuzi wa simu ya Infinix Hot S X521 na Bei yake nchini Tanzania

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako