Ifahamu simu ya Tecno Camon C9 bei na Sifa zake


Simu kali ya Tecno Camon C9 yenye uwezo wa hali ya juu katika kupiga picha ikiwa na Camera mbili (Mbele na nyuma) za Megapixel 13, uwezo wa 4G LTE na teknolojia mbali mbali za kisasa imeingia rasmi sokoni. Simu hii ni miongoni kwa simu za kisasa kuingizwa nchini, na inapatikana kwa bei ya kawaida ya Tsh.400,000.

Tecno Camon C9 ni mrithi wa Camon C8. Tecno Camon C9 ina kamera bora zaidi, prosesa inayofanya kazi kwa haraka, Android 6.0 (Marshmallow) na RAM ya 2GB.

Sifa kuu na uwezo wa Tecno Camon C9

  • Kioo:Ukubwa wa inchi 5.5, ubora wa kioo ukiwa 1080 x 1920 pixels
  • Uwezo: 1.3GHz octa-core Mediatek MT6753 CPU na RAM ya 2GB
  • Mfumo wa uendeshaji: Android 6.0 (Marshmallow)
  • Uhifadhi: 16GB ya uhifadhi wa ndani pia unaweza kuweka memori hadi 128GB
  • Kamera: Kamera ya nyuma ina 13MP na kamera ya mbele ni 13MP
  • Teknolojia nyinginezo: 4G LTE Data
  • Laini za simu: Inakubali laini 2
  • Betri: 3000 mAh ina uwezo wa kuchaji kwa haraka

Ubora na Kioo

Simu janja hii ya Android ina muundo tofauti na mtangulizi wake. Vitufe vyote sasa vimehamishiwa upande wa kulia.

Tecno Camon C9 bado ina kioo cha ichi 5.5 IPS, lakini sasa kina uwezo zaidi wa 1080 x 1920 pixels kwa uzoefu bora kuonyesha. C8 ilikuwa na saizi ya 720 x 1280 tu, hivyo hii inapaswa kuwa bora zaidi.

Kamera na Uhifadhi

C8 ilitengenezwa kwajili ya wapenzi wa picha na Tecno Camon C9 inaendelea urithi huo. Upande wa nyuma kamera bado inajumuisha megapixels 13, lakini usikosea sio kamera sawa na C8.

Tecno Camon C9
Tecno Camon C9 inakuja na kamera iliyoboreshwa zaidi. Simu imewekwa mfumo wa lens 6, lens moja zaidi kuliko mtangulizi wake. Hii inasababisha picha bora zaidi na uzalishaji bora wa rangi.

Kamera ya mbele pia imeboreshwa kutoka kamera ya megapixel 5 hadi kamera ya megapixels 13. Kamera ya mbele sasa ipo katikati.

Tecno Camon C9 pia ina kamera kwajili ya Iris scan. Kipengele hicho, ni sawa na kile kinacho patikana katika simu ya Lumia 950 kitakuwezesha kufungua simu yako kwa urahisi bila nenosir

Simu ina diski uhifadhi ya 16GB, ambapo unaweza kuiongeza kwa kuweka memori kadi ya hadi 128GB.

Vifaa na Programu

Tecno Camon C9 inatumia prosesa mpya. 8-core Mediatek MT6753 chipset yenye kiwango cha 1.3GHz ikiwa na pamoja na RAM ya GB 2 na inatumia Android 6.0 (Marshmallow).

Tecno Camon C9 ina betri lenye kiwango kizuri tuu cha chaji, nacho ni mAh 3000, kwa kiwango hichi basi utegemee si chini ya siku nzima ya bila kuchaji katika matumizi ya kawaida.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA